Waziri wa Afya amsimasha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road Dk.Diwan Msemo

Kasi ya Rais Magufuli na
kila serikali yake inachokifanya kwa sasa Waziri wa Wizara ya Afya na
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemsimamisha kazi kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk, Diwan Msemo ili
kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini mgongano wa
kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi hiyo chini ya kaimu mkurungenzi
huyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu imesema kutokana na ziara alizofanya Dk.Rais MAGUFULI inaonyesha kukosekana kwa dawa katika hospital za Serikali huku vituo vya afya binafsi vikiwa na dawa.
Taarifa ya Waziri hiyo imesema kuwa
upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya
wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu hatazile
wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinatakiwa kutolewa bure
na Serikali.
No comments