Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

MATUKIO NA HABARI- IDARA YA CA’s 2015 | ABDIEL SIFI




9/22/2015
MATUKIO NA HABARI- IDARA YA CA’s 2015 | ABDIEL SIFI
DSC07769.JPG


Text Box: CHRISTIAN AMBASSORS (CA’S) AMKA KIJANA-01.

 

Utangulizi:
Kanisa Kama taasisi linapaswa kuwa na mfumo wa utunzaji kumbukumbu.Lengo ni kutunza historia, kujipima kimaendeleo katika utendaji. Nikiwa Katibu wa idara ya vijana kanisa la KCC nimeaona ni vema kuandika kihabari zaidi mambo machache ambayo yametekelezwa na idara ya vijana 2015. Yaliyopo hapa ni machache kati ya mengi yaliyofanywa na idara Pamoja na Kanisa. Nimeyachagua machache kulingana umuhimu wake katika idara ya vijana na kanisa. Hata hivyo sisemi kuwa kila habari itamfurahisha kila mtu, la hasha! Wengine watachukizwa. Nikiwa mwanahabari Napenda kutoa angalizo na ulinzi wa kimaadili ya uandishi wa habari, kwamba majina ya vyanzo vya habari ambavyo vimeshiriki kutoa maoni katika baadhi ya mada hayajatajwa, kwa sababu ya kulinda utu, heshima zao.Izingatiwe kuwa maoni yao si kwa nia mbaya bali ni kujenga na kurekebisha. Ukusanyanji wa maoni umehusisha viongozi na washirika wa makanisa mabalimbali ya kiroho jijini Dar es salaam. Nia yangu ni kuona idara ya vijana inaendeleza jarida hili la AMKA KIJANA kila mwaka.
SHUKRANI:
Namshukuru MUNGU kuniwezesha kufanikisha kuandika jarida hili.
·         Mama mpendwa Mch. E. Mayala kwa ushirikiano alioutoa na  kukubali kuandikwa jarida hili.
·         Dada Janeth Kimei kwa kujitolea kuhakikisha jarida hili linachapishwa.
·         Nawashukuru waliotoa maoni juu ya mada mbalimbali, lakini hawatataja kutokana na sababu za kitaaluma.

MUNGU AWABARIKI SANA.


CHACHI.JPG
kanisa la KCC

DSC07422.JPG
Baadhi ya vijana KCC wakifurahia jambo.

  
VIONGOZ I WA IDARA YA VIJANA (CA,s).

                                 OO
Lena Mwavea M/kiti    CA’s                                 Yusuph Yona  Makamu M/kiti CA’s



Abdiel Sifi, Katibu CA’s.                                                                    Pendo Tarimo Mhazini CA’s




DSC09062.JPG
anaText Box: Wanapraizi wakiongoza sifa.
DSC07348.JPGDSC05228.JPGText Box:  Lazaro akikabidhi zawadi kwa Mwl wa  watoto 2015.Text Box: Robert na mkewe wakimshukuru Mungu kupata mtotovijana wakiwa kambini Kibaha


Ijue historia ya KCC.

Inawezekana wewe ni mshirika wa muda mrefu wa kanisa la Kibamba Christian Center (KCC), lakini hujawahi kusikia wala kuhufahamu historia yake. Kama yalivyo makanisa mengi kuanzia katika mazingira magumu, KCC ni moja wapo. Chimbuko la KCC lilianza 1986 katika shule ya msingi  Kibamba. Dominic Kihampa, Mwangalizi wa Seksheni ya Kibamba na mke wake ndio walianzisha huduma shule ya msingi Kibamba.Baada ya Mchungaji Dominic na familia yake kuhamishwa kikazi, kanisa aliliacha kwa Mch. Moses Mayala na mke wake 1993 likiwa shule ya msingi Kibamba. Mayala na mke wake walifanikiwa kufungua tawi Kiluvya kwa komba, mtumishi aliyekabidhiwa kuchunga kanisa hilo aliasi hali iliyozua mgogoro kati ya Mtumishi huyo na Kanisa la TAG. Hata hivyo kanisa hilo halikuendelea badala yake lilibadilika na kuwa KLPT Kiluvya ambalo lipo hadi leo.Mayala aliendelea na huduma mahali hapo hadi 1995, baada ya serikali kupiga marufuku shule za msingi kutumika kuabudia. Mch.Mayala na mke wake walitafuta eneo jipya kwa ajili ya kuendeleza huduma. Eneo lilipatikana mahali ambapo kanisa lipo hadi leo.
Washirika wasiozidi 30 walianza kujenga kanisa 1993 hadi 1995 ujenzi ukakamilika na kuwekwa- jiwe la Msingi 30, April 1995 na Askofu wa jimbo la Mashariki Magnus Mhiche. Kanisa la KCC limefungua matawi yafutayo, Kwembe, Hondogo, Kibamba Hospitali, Kibamba Njia Panda, Kisarawe. Waimbaji na watunzi wa Nyimbo za injili waliolelewa na KCC ni pamoja na Ruto Rafaeli na Neema Kipangula. 2004- 2005 kanisa lillipata Mwl, wa Kwaya Mr. Alipo ambapo kwaya ilifanikiwa kutengeneza albamu yenye nyimbo zaidi ya 16. Albamu hiyo bado haijazinduliwa wala kurekodiwa kanda za video kutokana na sababau mbalimbali. Kanisa hili huendesha ibada mbili kwa lugha kiingereza na Kiswahili. KCC inaongozwa na Mchungaji Moses Mayala, Ebia Mayala, Wachungaji wasaidizi Ibrahim Mkwiche na Isaack Kuderi. Katibu wa kanisa akiwa Mbonea Mtaita. Pia kuna idara zifuatazo, Idara ya Maendeleo, Uinjilisti, Maandiko, Kwaya, Sifa na Kuabudu, WWK, CMF, vjiana (CA’s), na Watoto.

Mama Mch, E. Mayala na Mwl Methew wakiwa na  vijana  katika huduma

Nini chanzo washirika kuhama Makanisa?.                               
Tabia ya washirika kuhama makanisa inazidi kukua ndani ya makanisa ya kiroho.Tabia hii isipokemewa na viongozi wa makanisa inaweza kuleta madhara kwa kanisa la mahali pamoja.Uchunguzi wa muda mrefu uliohusisha Wachungaji, viongozi wa idara, washirika wa makanisa mbalimbali ya kiroho, unatoa majibu yafuatayo. Kila kanisa la mahali pamoja lina historia yake, tangu kuanzishwa kwake, idadi ya watu walioanza huduma mahali hapo. Lakini hao hao ambao ni waanzilishi (washirika) baadae huhamia makanisa mengine sio kimakazi bali kusali katika makanisa hayo.Hali hii huzua maswali kwa wachungaji washirika na viongozi wengine kwanini mtu anahama kanisa. Zipo sababu mbalimbali ambazo husababisha mtu/watu kuhama katika hali ya kawaida,inawezekana kuwa mtu amehamishwa kikazi hivyo analazimika kuhama mahali anapoishi.Hapa tunazungumzia mtu ambaye hajahamishwa eneo la kazi bali anaishi eneo lilelile lakini anahama kanisa. Maoni ya watu waliohojiwa yanajikita katika pande mbili kama ifuatavyo. Sababu za mtu mwenyewe, pili ni mfumo wa utawala ndani ya kanisa.
 Sababu za mtu binafsi
Jada mkomba (sio jina lake), anasema “watumishi ndani ya kanisa kutokuwa na vifua/ uwezo wa kubeba matatizo/siri za washirika, unakuta mshirika anapitia mambo magumu na  anapomshirikisha kiongozi ndani ya kanisa, badala ya kuhifandhiwa matatizo yake hugeuzwa kuwa mahubiri kanisani. Jambo hili linaweza kumkera mtu kutotunziwa siri zake hivyo kuamua kuondoka”. Anaendela kusema washirika wenyeji  kutokujali washirika wapya, upendo wa kweli kupungua miongoni mwa washirika. Matabaka ndani ya kanisa, wenye pesa na wasio kuwa nazo. Hivyo mtu ambaye kipato chake ni kidogo anapopatwa na matatizo ushirikiano anaoupata kutoka kwa washirika ni mdogo kuliko ule anaoupata mtu mwenye kipato cha juu.Kibaya zaidi ni washirika kufanya dhambi ya usengenyaji,fitina, wivu, husuda, kutetana,inachangia sana kuwaondoa watu katika kanisa la mahali pamoja.Kinachotakiwa ni kuwasaidia na kuwaombea kwani kwa kuwasema haiwezi kusaidia wao kuondokana na udhaifu walionao” anasema Jada. John Nangwa (sio jina lake) ambaye ni katibu wa idara ya vijana katika kanisa fulani Bagamoyo anasema “kitu ambacho kinasababisha watu wahame makanisa ni kuwa na  imani finyu, watu huhama makanisa wakitafuta miujiza ya uponyaji na mafanikio bila wao kuwa na juhudi ya kuutafuta uso wa Mungu”. Ghula Simon- anasema kanisa likiwa na viongozi wasioelewana kutoheshimiana, uzinzi, na tabia zingine chafu husababisha kuhama kwa waumini waaminifu na wanaopenda kuona maendeleo ya huduma yanakuwa mazuri. Maana maendeleo hayawezi-kupatikana kanisani ikiwa viongozi hawaelewani na kusikilizana. Kanisa likiwa na uongozi dhaifu (wazee wa kanisa  na idara) kukosa mikakati mizuri ya kimaendeleo kiroho, huduma, kiuchumi, na kimwili kwa mtu anayependa mambo haya yaonekene hawezi kuvumilia kuishi ndani ya kanisa kama hilo”.kuna aina nyingine ya watu kuhama, wakati ambapo kiongozi wa juu kanisani akihama, washirika dhaifu wa imani huunga behewa kufuatia sababu ambazo huyo kiongozi zilisababisha yeye kuhama, hasa ikizingatiwa kuwa kiongozi huyo aliheshimika na kupendwa kanisani anasema Ghula.

Sababu za mfumo wa utawala
Mchungaji Kilio kalemela (sio jina lake) anasema “Hapo zamani kulikuwa na utaratibu wa kanisa la TAG wa kupokea wageni, ambao siku hizi hauzingatiwi sana na viongozi wa kanisa. Ilikuwa lazima mtu anayehamia kuwa na barua ya utambulisho wa kanisa analotoka ambayo huiwasilisha kanisa analohamia.Utaratibu huu hauzingatiwi hivyo mgeni hupokelewa bila barua, badala yake hujieleza tu kwa viongozi wa kanisa na kupokelewa. Maelezo pekee hayatoshi- kuaminika kwamba taarifa zake ni sahihi au la!. Lakini pia jitihada za makusudi hazifanyiki kujua ni wapi alipotoka ili kujiridhisha. Hivyo, akiamua kuodoka anaondoka tu! tena bila kuaga, anasema Mchungaji Kalemela. “Tabia ya washirika kuhama makanisa inaendelea kukua na kupanuka hasa makanisa ya mijini na isipoangaliwa kwa makini itabasabisha kanisa kutoendelea na kukua katika huduma maana watu wamebeba huduma ambazo zingekuuzwa na kulelewa mahali pamoja zitaimarika zaidi na kukua.  Mchungaji Kilio anataja sababu nyingine kuwa demokrasia ndani ya kanisa ni muhimu ikawepo, viongozi, washirika kuwa na uwezo wa kuhoji, kukosoa na kutoa maoni yao juu ya mambo yanayohusu kanisa.Mgawanyo wa majukumu lazima uzingatiwe ndani ya kanisa. Unaweza kukuta Mchungaji Kiongozi anakuwa na majukumu mengi kupindukia hali inayosababisha kuzidiwa na kushindwa kumudu. Usaidizi ni Mzuri kama ambavyo alifanya Musa kwa kuwateua Maliwali na Maakida ili wamsaidie majukumu ikiwemo kusikiliza na kutatua matatizo yao.Kanisa ni taasisi ambayo inatakiwa kuendeshwa kiitifaki/kila kiongozi awe na mamlaka ya kusimamia majukumu yake bila kuingiliwa.Wachungaji kuwa waamuzi wa kila jambo unafanya viongozi wengine wa idara kumtegema mchungaji.Hii inasababisha viongozi wa idara kutojitegemea kimaamuzi katika nafasi zao” anasema.

Sababu nyingine ni kutojali watu wenye huduma au wito maalum. “Mungu ametupa vipawa na uwezo tofauti kila mmoja, inapotokea mtu anahamia ndani ya kanisa akiwa na wito katika huduma fulani hukosa nafasi ya kufanya huduma hiyo. Ikihofiwa kwamba anaweza kuwakosesha nafasi waliokuwepo kuhudumu. Mtu wa namna hiyo kwa kuwa anajua kumtumikia Mungu katika huduma yake hawezi kuendelea kudidimiza huduma hiyo bali atatafuta sehemu ambayo anaweza kutumika”.Washirika hupatikana kanisani kwa njia mbili kuu,ushuhudiaji na kuhamia. Hivyo kanisa lina wajibu wa kuhakikisha lina kuwa na utaratibu wa kuwachunga watu wake, kuwasilikiza  pamoja na kuwafundisha huduma na kutumika.Hii itasababisha mtu kuwa na imani ya kweli  na Mungu anayemwabudu na kubaki kanisani na sio kutanga tanga akitafuata Miujiza. Akinukuu biblia Takatifu “Mithali 14: 28 (utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake, bali uchache wa watu ni uharibifu kwa mkuu wao )” Hivyo kanisa linapokuwa na watu wengi maana yake ni Utukufu kwa Mungu na Mchungaji. Mungu anapenda watu wakusanyike kwa wingi wamwabudu na kumsifu yeye katika roho na kweli, kinyume chake ni uharibifu.

Nini kifanyike.
Kutokana na changamoto hizi zinazokabili makanisa ya kiroho, kunahitajika mambo kadhaa kuzingatiwa ili kuondoa tabia ya watu kuhama makanisa badala yake wakuuzwe kulelewa na- kuendelezwa kwa huduma zao ili kuleta mandeleo ya kiroho na kimwili ndani ya kanisa.Kwanza kabisa ni lazima kanisa liwe na mfumo wa kisasa wa kupokea wageni na kuwalea vizuri,Wachungaji, wazee wa kanisa na Wakuu wa idara washirikiane kuhakikisha wageni wanalelewa vizuri na kukuzwa kiroho.Kuwajali washirika na kudumisha upendo, kusikiliza mahitaji na kuwatunzia siri na matatizo yao. Kuwa na uongozi thabiti unaojikita katika mipango mikakati mizuri ya kukuza huduma na kuondoa matabaka ndani ya kanisa, kwamba wenye pesa na wasio kuwa nazo wawe kitu kimoja katika mwili wa Kristo ili kuleta uhai wa huduma iliyosimama imara. Kwa kufanya hivyo kanisa litakuwa kama taa inayoangaza gizani na kuwavuta watu.


Mchungaji awataka vijana kuacha uzembe.
Mchungaji Msaidizi Pasco Masawii wa kanisa la TAG Maili Moja amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha uzembe ili waweze kujikwamua kiuchumi. Alisema hayo wakati akifundisha vijana katika kambi ya wiki moja ya vijana iliyoshirikisha vijana 104 kutoka seksheni ya Mbezi na Kibamba iliyofanyika Wilayani Kibaha kuanzia Julai 22-27 2015.“Inashangaza kuona vijana waliookoka wamebweteka tu, -hawajishughulishi na kazi hali inayosababisha kuwa nyuma kimaendeleo ya kiroho na kimwili.Watu wanaopenda kupata kirahisi, wavivu na wenye aibu ya kufanya kazi.Tabia hii ndio chanzo cha kudhaulika katika jamii na kwamba hata wokovu wao hutiliwa mashaka.”[i]Mchungaji Masawii aliwaeleza vijana kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, ili kujijengea sifa njema na kwamba inapofika wakati wa kuoa au kuolewa ni rahisi kwa sababu msichana / mvulana hupenda kuoa / kuolewa na mtu mchapa kazi, mwenye hofu ya Mungu. Akitolea mfano kijana Simon Mwashiuya kutoka TAG Kibamba (KCC) ambaye alifika kambini akiwa na karanga kwa ajili ya biashara, kuwa ni kijana anayejituma na kujishughulisha hivyo Mungu lazima atamwinua.Mchungaji Masawii aliitisha changizo kwa ajili ya kumwongezea mtaji ambapo zaidi elfu 50,000 zilipatikana. Pamoja na hayo Mchungaji aliwaonya vijana wote kujiepusha na vitendo viovu badala yake wamtumikie Mungu kwa uaminifu.



_________________________________________
Badiliko la kiroho huleta haki Kwa Taifa.
Kwa upande mmoja (ukizingatia utawala wa Warumi) kuna wanaotoa maoni kwamba Yesu wa Nazareti alikuwa na makosa.Kwamba alijiita- masiha na alikuwa na- mpango wa kuupindua utawala wa Warumi. Wanasema Yesu wa Nazareti, alianzisha vuguvugu la kisiasa na kidini (Religion-political movement).Kwamba hata yeye hakuwa tofauti na makundi mengine yaliyokuwa yakipigania Uhuru wa Israeli, kama vile Zealots na wengine.Kati ya wafuasi wake walitoka kwenye makundi haya ya wapigania uhuru: “Matayo na Toma, Yakobo na Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zeloti), Yuda Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa mhaini” (Luka 6:15-16).Kwamba yeye alisisitiza ufalme wa kiroho. Ya Kaizari yaende kwa Kaisari na ya Mungu yaende kwa Mungu. Kwamba- mafundisho yake yote yalikuwa ni ya kiroho. Mashtaka ya kisiasa juu yake yalipikwa na viongozi wa Wayahudi waliomchukia. Hata hivyo, Ukweli juu ya Yesu wa Nazareti, haukujikita kwenye maoni ya pande hizi tofauti. Pia, kuna ukweli kwamba Wayahudi hawakutofautisha siasa na dini.Kile ambacho leo tunakiita siasa, masuala ya kijamii, uchumi na dini, kwao ilijulikana kama Mungu na sheria. Hakuna kitu chochote katika jamii ile ya Wayahudi kilichojitegemea bila kuegemea kwa Mungu na sheria.Mungu, aliyaongoza maisha yao, aliwalisha, aliwanywesha, aliwalaza na kuwaamsha, aliwaelekeza la kufanya na kuacha, aliwahamisha kutoka nchi hadi nyingine na mwishowe aliwapatia nchi nzuri yenye maziwa na asali! Alikuwa Mungu wa wivu!. Hakutaka wawe na uhusiano na miungu wengi, au wafanye mambo yasiyompendeza. Hivyo siasa kama siasa tunavyoifahamu leo hii haikuwepo katika maisha ya jamii ya Wayahudi. Ndiyo maana walipigana kufa na kupona kuondoa utawala wa Warumi uliokuwa ukitenga siasa na dini. Yesu wa Nazareti, alitaka kuikomboa Israeli kutokana na utawala unaotenga dini na siasa. Lakini yeye alikuwa na maoni tofauti na wengine. Yeye aliamini kwamba- ukombozi huu ungewezekana kama Israeli ingebadilika kutoka rohoni. Ni lazima kubadilika kutenda wema, haki na huruma. Bila hivyo hata kama wangefanikiwa kuwapindua na kuwafukuza Warumi, watawala wa Kiyahudi wasingekuwa tofauti.Yesu wa Nazareti alionyesha waziwazi kwamba maisha ya kitabaka yaliyokuwa miongoni mwa jamii ya Wayahudi yalikuwa ni ya kiunyanyasaji zaidi ya utawala wa Kirumi. Hivyo la msingi siyo kubadilisha utawala, bali ni kubadilisha roho za watu, bila kufanya hivyo hakuna ukombozi wa kweli!. Hapa ndipo kuna somo hata kwetu sisi hapa Tanzania. Watu na wanasiasa wamekuwa na hamu na shauku ya kubadilisha utawala kutoka CCM na kwenda kwa vyama vingine ili kuleta mabadiliko katika utendaji na kupambana na rushwa na ufisadi.Maaskofu wetu wanafikiri elimu ya uraia inaweza kusaidia kupambana na rushwa na ufisadi. Kama ilivyokuwa wakati wa Yesu, hata sisi mabadiliko yetu hayawezi kuleta matunda mema, kama hakuna mabadiliko kutoka rohoni. Ni lazima kwanza Tanzania, ibadilike kutoka rohoni. Ijenge kwanza mifumo ya kuhimiza matendo ya wema, haki na huruma. Kinyume na hapo, hata vyama vingine vitatenda kama ilivyokuwa ikitenda CCM! Wale wote wanaolilia mabadiliko ni lazima walifahamu hili kwanza ndipo tusonge mbele. Vinginevyo tutabaki palepale!.Utawala wa Kirumi, ulimaanisha kulipa kodi ya Kirumi; kama ulivyo utawala wowote hapa duniani. Kodi ni kitu kinachotangulizwa!.Kwa Wayahudi kulipa kodi kwa Warumi kulimaanisha kumpatia Kaizari vilivyo vya Mungu: Yaani Israeli na mali zake zote. Yesu alikuwa na maoni tofauti: “Basi, baadhi ya Wafarisayo na Waherodi walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake. Wakamwendea, wakamwambia, ‘Mwalimu, tunafahamu kwamba wewe ni mtu anayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu ye yote. Wala hujali cheo cha mtu lakini huwafundisha ukweli kuhusu njia ya Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaiaziri au la! Tulipe au tusilipe’? Lakini Yesu akijua unafiki wao akawaambia, ‘Mbona mnanijaribu? Nionyesheni sarafu’ Wakamwonyesha.Naye akawauliza, ‘Picha na chapa hii ni vya nani?’ Wakajibu, ‘Ni vya Kaisari’. Basi, Yesu akawaambia, ‘Mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari na Mungu vilivyo vyake Mungu”...(Marko 12: 1-17).Fedha zilikuwa na picha ya Kaisari, hivyo kukataa kumpatia kodi Kaisari ni ishara ya kupenda fedha na mali. Ili kumpatia Mungu, vilivyo vya Mungu ni kuuza vitu vyote na kuwapatia fedha maskini, ni kuachana na tamaa ya kupenda madaraka na kuishi kwa anasa. Somo hapa ni kwamba Kwa Mungu, hakuna fedha, kwa Mungu, hakuna kuuza na kununua. Kwa Mungu kuna kupewa bure na kutoa bure.Hiyo ndiyo changamoto ya maisha ambayo hadi leo hii iko mbele yetu. Kuuza na kununua siyo utamaduni wa wale wanaomfuata Yesu wa Nazareti.Utamaduni wao, ambao ulijengwa na mwanzilishi wa- imani hii, ni kutoa bure, maana tunapokea bure kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Pia, utamaduni wa kuuza na kununua siyo wa Mungu. Sote, tunapokea vipaji, tunapokea maisha bure kutoka kwa Mwenyezi Mungu – hakuna anayelipa chochote ili kuupata uhai, hakuna anayelipa chochote ili kupata vipaji, akili, hekima na busara.Yote tunapewa bure na tunaagizwa kutoa bure! Bila kutenga dini na siasa, jambo hili linawezekana! Mungu, akiwa kiongozi wetu – na siasa zote zikachipuka kutoka kwa Mungu tunaweza kuendeleza sera ya:“Tumepewa bure na tutoe bure” – sera ambayo inaweza kujenga amani ya kudumu hapa duniani. Vita na mapambano yote tunayoyashuhudia hivi leo ni kwa sababu dunia ilijiingiza kwenye mfumo wa kuuza na kununua.Jambo hili linaitesa dunia na litaendelea kuitesa, hadi pale tutakapotambua mafundisho ya Bwana Yesu wa Nazareti ya kupewa bure na kutoa bure,Wenye vingi, wanataka kuwauzia wenye vichache, lakini siyo kuwauzia bali kutaka kuwatawala kimawazo na kiuchumi.Mungu. Hapo ndipo mapambano yanaanza, maana kila mtu ameumbwa na uhuru wake na daima kuna kishawishi cha kutetea uhuru huu. Inawezekana wengine wakapigana na kuupata uhuru, lakini bila mabadiliko ya rohoni, uhuru wao unakuwa hauna maana yoyote, hata wanaopata uhuru wao, wanaendelea kunyanyasana wao kwa wao. Hoja ya msingi aliyoishughulikia Yesu wa Nazareti ni unyanyasaji, siyo kwamba wakoloni Warumi waliitawala Israeli. Yeye aliguswa na unyanyasaji uliokuwa ukiendelea miongoni mwa jamii ya Wayahudi. Aliguswa na umaskini, magonjwa, njaa na ubaguzi wa kupindukia. Hakuangalia kama anayesababisha yote hayo ni Mkoloni Mrumi au Myahudi. Aliuchukia uovu! Jamii yoyote ile ikiwa na utamaduni wa unyanyasaji na ubaguzi, hata kama si ya kikoloni – haimpendezi Mwenyezi Mungu.Wale waliopinga utawala wa Warumi na kuendeleza unyanyasaji na ubaguzi miongoni mwa jamii ya Wayahudi hawakuwa na tofauti na wakoloni Warumi. Hivyo, Yesu alibadilisha mwelekeo wa mapambano kutoka kupinga utawala wa Warumi na kuelekeza mapambano kwenye kutetea maskini na wenye dhambi. Huu ni msimamo tofauti na wa wale waliokuwa wanapigania utaifa wa Israeli, upekee wa Wayahudi, upekee wa dini ya Wayahudi, ubora wa Wayahudi na kwamba wao ni taifa teule. Huu haukuwa msimamo wa ukombozi wa kweli. Ukombozi wa kweli, kama alivyoonyesha Yesu wa Nazareti, ni kuuthamini ubinadamu. Kumpenda adui ni msimamo wa kuthamini mshikamano wa binadamu wote.

Makala hayo hapo juu yamenyofolewa kutoka tovuti ya www.mwananchi.co.tz yaliyoandikwa na Privatus Karugendo Machi 2015.yamewekwa hapa kutoka na umuhimu wake kiroho

Mch. Mkwiche: Tunapaswa kuombea Taifa letu.
“Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2015, tumeshudia Taifa letu likikabiliwa na matatizo mengi ambayo yanatukumbusha wajibu wetu wa kumwomba Mungu haya ayasiendelee kutokea” ni maneno ya Mchungaji- msaidizi Ibrahim Mkwiche wa Kanisa la Kibamba Christian Center (KCC). Akiyataja baadhi ya matatizo yanayoendelea kulitesa Taifa, ni kuongezeka kwa ajali za barabarani, mauaji ya albino, na utekaji wa watoto.“ Ajali iiyotokea mkoani Njombe iliyohusisha basi la Majinjah kugongana na lori la mizigo iliua zaidi ya watu 50, ajali zingine mbili zilizotokea mkoani Morogoro, ziliangamiza watu zaidi ya 20, kufungiwa kwa watoto 18 wilayani Moshi na mauaji ya Albino yanayoendelea katika sehemu mbalimbali nchini, yanaashiria ni namna gani watu wamekuwa wakatili waovu na waonevu, hali hii haivumiliki kwa Mungu hata Kidogo.Tunao wajibu kama watu- wanaomwamini Mungu na wenye mapenzi mena na nchi yetu, hivyo tunapaswa kuliombea Taifa letu ili Mungu aepushe haya yasiendelee kutokea” alisema.Ikiwa watu wanaomwamini Mungu hawatachukua hatua stahiki kwa kuliombea Taifa basi ni Vigumu Mungu kuiponya na akuibariki nchi kama ailivyoandikwa katika biblia 2Nyakati7:14  ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha na- kuomba na kuutaafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kusamehe nchi yao na kuiponya nchi yao.Katika hali ya kawaida lazima tujiulize kama Taifa, kama waumini na kama wananchi kwanini haya yanatokea.Ndugu zetu wanauawa kwa imani za kishirikina,wengine wanapoteza maisha kwa ajali,kukithiri kwa vitendo vya kikatili na viovu, bila shaka ni kwa sababu tunamkosea  Mungu na hivyo anatupa onyo ili tumrudie yeye. Kwa maana hiyo hawezi kuibariki nchi na watu wake ikiwa hawajajisahihisha kwanza. Hata hivyo aliwaomba washirika kuomba Mungu kwa bidii sana wakati huu Nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu ili kupata viongozi ambao watafaa na kuongoza Taifa katika misingi ya haki na usawa.
_________________________________________
Hongera Mchungaji Moses Mayala.
Katika kuhakikisha kuwa huduma ndani ya kanisa TAG Kibamba zinapanuka Mchungaji Kiongozi Moses Mayala alianzisha ibada kwa lugha mbili tofauti Ibada ya kwanza kwa lugha ya kiingereza ambayo huanza Saa 1:00 kila jumapili ikiwalenga watu wanaopendelea kupokea neno la Mungu kwa Lugha hiyo. Pia ibada ya Kiswahili ambayo huanza saa 4:00 asubuhi kila- jumapili.Kuwepo Kwa ibada hizi mbili kwa lugha tofauti kumetoa uhuru wa watu kuabudu kwa lugha anayoipenda.
DSC08343.JPGKatika kuhakikisha vijana wanakua katika huduma kanisani Mchungaji ametoa nafasi pana kwa vijana kuhudumu katika ibada hizi.Hata hivyo ibada zote hizi zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kuepukwa mara moja. Moja na kubwa ni washirika kuchelewa ibadani hali ambayo inasababisha ratiba za ibada kutofuatwa kama inavyotakiwa.

__________________________________________
CA’s   ya KCC yang’ara.


Mwanzoni mwa mwaka huu, viongozi wa kanisa kushirikiana na idara zote kanisani wamewezesha vijana kushiriki katika mikutano na semina mbalimbali zilizoandaliwa nje na ndani ya kanisa, Seksheni, na Jimbo. Katika semina ya wiki moja iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu kanisani iliyoshirikisha vijana zaidi ya 50 ambapo walifundishwa masomo kama mahusiano, uchumba na ndoa na maadili ya kijana aliyeokoka. Mwalimu aliyesimamia semina hiyo Mama Methew alikiri kufurahishwa na ushiriki wa vijana katika
semina hiyo.Mwezi July vijana nane walishiriki katika kambi ya Seksheni ya Kibamba na Mbezi iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mwenyekiti wa vijana Lena Mwavea amekuwa mstari wa mbele amasisha vijana kushiriki fursa mabalilmbali kujifunza neno, huduma na kumtumikia Mungu, ambaye pia alikuwemo katika kambi hiyo. Wengine waliohudhuria ni Katibu wa vijana Abdiel Sifi, Mhazini wa idara Pendo Tarimo, Mpiga gitaa maarufu Jeremiah Mayala, David Traifon, Emanuel Mbwambo, Salome Mayala na Simon Mwashiuya. Hata hivyo vijana wa KCC waliibuka vinara katika kambi hiyo baada ya kuonesha uwezo katika mambo tofauti, Emmanuel Mbwambo alionesha umahiri mkubwa katika utunzi wa igizo ambalo lilichukua nafasi ya kwanza. Naye katibu wa vijana Abdiel Sifi alionesha kipaji cha Utangazaji baada ya kutangaza habari zote zilizotokea katika kambi hiyo. Kubwa zaidi ni baada ya  Simon Mwashiuya kunyookewa na mkono wa Mungu na kukusanya zaidi ya elfu 50 kuongezea mtaji wa biashara yake ya karanga.Idara hiyo pia imeshiriki matukio makubwa ya kitaifa ambapo mwezi Agosti Vijana waliaonesha moyo wa kumpenda Mungu kwa kuchangia zaidi ya shilingi 100,000 ili kumuewezesha kiongozi mmoja awakilishe  idara katika mkutano wa vijana kitaifa uliofanyika Mjini Dodoma. Jimbo la Mashariki kaskazini lilishika namba moja katika majimbo yaliyopeleka wajumbe wengi zaidi. Nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Jimbo la Mashariki Kusini.
___________________________________________







Hitimisho
Napenda kumshukushuru Mch.Moses Mayala, Ebia Mayala na viongozi wote wa idara zote kwa  kazi kubwa wanayofanya kutulea vijana na kanisa.
Shukrani kwa timu ya sifa na kuabudu (praise & worship team) chini ya Daniel Mayala kwa bidii kubwa ya kumtumkia Mungu.
Washirika wote kwa umoja wao.
Zaidi ya yote kama kanisa tudumu katika upendo na tusikate tamaa pia kuonyanyana katika jina la Yesu.
Upendo na udumu katika ndugu: Ebr . 13:1


Kambi ya seksheni Mbezi & Kibamba Jully 2015
Kambi ya kitaifa ya viongozi CA’s  Agosti 2015, Dodoma.
Maoni ya viongozi mbalimbali katika makanisa ya kiroho.



No comments