Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake

nguvu za kiume
429
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha mwisho cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.

Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake

Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.
Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Soma zaidi kuhusu mazoezi hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;
  • Umri wa mgonjwa
  • Jumla ya afya aliyonayo kwa kwa sasa
  • Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
  • Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k
  • Ni nini malengo ya tiba ?
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako, kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya tatizo linalokukabili.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii yaweza kumuacha mwanamke akiwa hakutosheka.
Mke wako hupendelea ukawie ikibidi ukawie zaidi. Kama mwanaume atakuwa anawahi kumaliza, basi anakuwa hampi raha mke wake.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.
Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili.
Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
  • Wasiwasi
  • Hofu
  • Msongo/Stress
  • Hasira
  • Huzuni
  • Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa
Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
  1. Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
  2. Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
  3. Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
  4. Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea pia kama kipengele kimojawapo katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo sawa. Pia sababu zingine za kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au kuwahi kufika kileleni ni pamoja na;
  • Umri mkubwa zaidi
  • Kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Kukosa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Maradhi ya moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
  • Kiwango kidogo cha homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa

Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Nini kinachofanya uume usimame? Kwa haraka unaweza kusema ni msisimko. Ndiyo, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha kutokea kwa msisimko huo. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu la swali hili ili atakapoona tatizo ajuwe wapi pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama wanavyodhani watu wengi.
Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.
Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri unywe maji bila kusubiri kiu.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu ulio katika afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili hii ikijumuisha pia damu ya kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kuwa hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Hebu mwangalie mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna, bonyeza hapa => Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko/Stress.
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Vyakula vinavyotibu tatizo la nguvu za kiume ni pamoja na vifuatavyo:

Tangazo:
Book Your Hotel Here:


1. Kitunguu swaumu

dawa ya nguvu za kiume
Kitunguu Swaumu
Chukuwa punje 8 mpaka 10 hivi za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.
Unafahamu kuwa kitunguu swaumu ni dawa ya zaidi ya magonjwa 30 mwilini? Soma magonjwa hayo yanayotibika kwa kutumia kitunguu swaumu kwa kubonyeza hapa => Kitunguu Swaumu Hutibu Magonjwa 30.

2. Tikiti maji

nguvu za kiume
TikitiMaji
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.  Soma faida nyingine 13 za tikiti kiafya kwa kubonyeza hapa => Faida 13 za Tikiti Maji Kiafya.

3. Ugali wa dona

dawa ya nguvu za nguvu
Ugali wa Dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

4. Chumvi ya mawe

tatizo la nguvu za kiume kwa wanaume
Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.
Kama unataka kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu umhimu wa chumvi mwilini, bonyeza hapa => Ukweli kuhusu Chumvi na Maajabu yake.

5. Maji ya kunywa

Chanzo cha kupungua nguvu za kiume
Maji ni Uhai
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.
Soma maajabu mengine ya maji kiafya kwa kubonyeza hapa => Jitibu kwa kutumia maji mp3.

6. Mbegu za maboga

Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 100 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako. Sasa, hizi usizitumie tu kama dawa, zitumie kama chakula na hivyo ziwepo tu nyumbani muda wote na kila siku uzitafune iwe unaumwa au hauumwi.

7. Asali na Mdalasini

tatizo la nguvu za kiume
Asali & Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali ndani yake. Unaweza kuitumia asali kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari.
Soma kazi nyingine 27 za kushangaza za asali yenye mdalasini mwilini kwa kubonyeza hapa => Asali na Mdalasini.

8.Chai ya TANGAWIZI

Chai ya Tangawizi
Chai ya Tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!

9. Unga unga wa udishe

tatizo la nguvu za kiume
Unga wa Udishe
Unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume. Udishe inapatikana pia katika mfumo wa juisi. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama.
Udishe pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.
Udishe unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika nguzu za kiume.
Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, udishe unapokuja kukutibu inakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.
Na iwapo utatumia juisi ya udishe basi vitu vingine vyote hapo huhitaji kuvitumia isipokuwa ugali wa dona ambao ni lazima kila mwanaume ale na siyo ugali wa sembe ambao hauna thamani yoyote mwilini.
Namna ya kutumia udishe –
Kama ipo katika mfumo wa unga: – Chemsha maji nusu lita ongeza kijiko kidogo cha chai cha unga huu, unaweza kuongeza pia asali vijiko viwili au vitatu na unywe kama chai kutwa mara 2, yaani asubuhi nusu lita na jioni tena nusu lita nyingine.
Kama ipo katika mfumo wa juisi:- Ukiamka asubuhi unamimina dawa robo lita ya dawa (ml 250), unakunywa yote na jioni tena robo lita nyingine, na dozi moja inachukuwa siku 11.
TAARIFA MHIMU – Juisi ya udishe ndiyo nzuri zaidi kuliko unga wake sababu inakuwa ni fresh zaidi, na wanaume wengi waliotumia juisi wanarudisha majibu mazuri zaidi kuliko wale waliotumia unga, hivyo kuanzia sasa udishe inapatikana katika mfumo wa juisi tu. Hivyo ukija WhatsApp au ukituma sms uliza moja kwa moja ‘Juisi ya Udishe ipo’?.


Unahitaji juisi ya udishe, Asali yenye mdalasini  au mbegu za maboga? Niachie ujumbe kwenye WhatsApp kwenye namba +255 769 142 586,  au niachie ujumbe wa kawaida (sms), Najibu haraka zaidi kama utanitafuta kwenye WhatsApp.
Kama hauna WhatsApp hadi sasa nakupa pole sana!. Ukiona nimechelewa sana kukujibu usiache kunitafuta tena hata siku inayofuata.
Kama huhitaji dawa yoyote ila unahitaji kuniona binafsi, weka miadi (appointment) kwa kubonyeza hapa.


Baadhi ya maswali ninayoulizwa mara kwa mara
1. Utajuaje mke au mpenzi wako amefika kileleni?
Kupata jibu la swali hili, bonyeza => hapa
2. Je, Mwanaume anatakiwa kuwa na uume wa ukubwa gani?
Kupata jibu la swali hili, bonyeza => hapa
3. Je Kuna Faida au Hasara ya Kupiga Punyeto au Kujichua?
Kupata jibu la swali hili, bonyeza => hapa
4. Je Mwanamke niliyenaye anaweza kuwa sababu ya mimi kuishiwa nguvu za kiume?
Kupata jibu la swali hili, bonyeza => hapa

Unahitaji juisi ya udishe, Asali yenye mdalasini  au mbegu za maboga? Niachie ujumbe kwenye WhatsApp kwenye namba +255 769 142 586,  au niachie ujumbe wa kawaida (sms), Najibu haraka zaidi kama utanitafuta kwenye WhatsApp.
Kama hauna WhatsApp hadi sasa nakupa pole sana!. Ukiona nimechelewa sana kukujibu usiache kunitafuta tena hata siku inayofuata.
Kama unahitaji kuonana na mimi binafsi, weka miadi (appointment) kwa kubonyeza hapa.

Kama kuna ambalo hatujalizungumzia hapa, tafadhari uliza swali kwenye comment hapo chini sasa hivi. Jibu la swali lako laweza kuwa msaada kwa wengine zaidi, hivyo niulize lolote kupitia boksi la comment hapa chini.

TANGAZO MHIMU:
Afya Kila Siku Group
Afya Kila Siku Group
Unatumia WhatsApp? Kama ndiyo jiunge na group langu la WhatsApp liitwalo “AFYA KILA SIKU” na upate dondoo za afya kila siku kwenye simu yako, pia utaweza kuuliza swali lolote muda wowote kuhusu jambo lolote linalokusibu kiafya. Ili kujiunga, pata maelezo kwa kubonyeza => HAPA.

No comments