Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ghana na ubora wake mwingine kwenye ligi kuu Uingereza!!

 
Nahodha wa timu ya Taifa ya Ghana na Mshambuliaji wa klabu ya Swansea City Andre Ayew amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita katika ligi kuu ya Uingereza.
Ayew mwenye miaka 25 amefunga magoli matatu msimu huu huku klabu yake ikiwa haijapoteza mchezo wowote msimu huu.
Swansea inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, ikiwa na pointi nane, baada ya kucheza mechi nne.
Manchester City ipo kileleni ikiwa na pointi 12 ikifuatiwa na Crystal Palace na Leicester  zote zikiwa na alama tisa.

No comments