Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Good news nyingine kwa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF  pamoja na afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wamburawametangaza September 9 kuingia katika makubaliano ya udhamini na mfuko wa Bima ya afya kwa ajili ya wachezaji wa Ligi Kuu  na viongozi.
TFF wamethibitisha mpango huo, mkataba watasaini hivi karibuni kwani unadhumuni la kulinda afya za wachezaji, kupitia kwa msemaji wa mfuko wa Bima wa taifa Singuamethibitisha mpango huo wa kuingia mkataba  wa udhamini kwa vilabu vyote 16 vitakavyoshiriki Ligi Kuu.
                                                   DSC_0059
Singu kushoto, Wambura kati kati pamoja na Mwesigwa Selestine
Mpango huo ni kuwa wachezaji 30 wa Ligi Kuu na viongozi saba ambao wapo klabu moja watapata nafasi ya kupata kadi ya Bima ya afya bure bila kuchangia chochote, hii ni kutokana na mkataba huo wa udhamini utakaosainiwa na TFF kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu.

No comments