Juventus wafanya umafia kwa Man Utd wenye hamu ya kujiboresha
Juventus wafanya umafia kwa Man Utd wenye hamu ya kujiboresha
Juventus wafanya umafia kwa Man Utd wenye hamu ya kujiboresha
Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus wametunisha msuli kwa kuikataa ofa ya klabu ya Man Utd ambayo ilikuwa na lengo la kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Chile Arturo Vidal.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo la nchini Italia Gazzetta Dell Sport Juventus wamekataa ofa ya Euro million 43, ambayo walikuwa wanaamini ingetosha kuweka ushawishi wa kufungua mazungumzo ya kumsajili Vidal.
Kukataliwa kwa ofa hiyo kunaelezwa kama sababu nyingine kwa Juventus kuonyesha dalili za kuendelea kubaki na mchezaji huyo, ama kumuuza kwa ada kubwa ya usajili ambayo huenda wakaitumia kwa kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya wawili.
Lakini kwa upande wa Man Utd ambao unapewa ushawishi na meneja kutoka nchini Uholanzi Louis van Gaal, haujazungumza lolote juu ya suala la kuwasilishwa kwa ofa huyo huko mjini Turin.
No comments