SOKOINE IS BACK IN TANZANIA
Anaitwa Patrick Ole Sosopi. Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa
Iringa, jimbo la Ismani. Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya
kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha
Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake ni kufuga ng’ombe. Ni Baba wa mke mmoja
na mtoto mmoja. Ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA
Bara- Taifa. Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna
shaka katika vipindi mbalimbali vya
maisha yake. Historia yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi,
sekondari hadi chuo kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye
serikali ya wanafunzi 2011/2012. Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009
alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho
kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na changamoto
mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili. Ole Sosopi ni mojawapo wa
waanzilishi wa CHASO mkoani Iringa, harakati zake katika jimbo la Ismani
na mkoa wa Iringa kwa ujumla kila mtu anazijua. Ameshiriki katika
mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja
na Mbeya. Wakati Daudi Mwangosi akiuliwa kikatili na jeshi la Polisi
alikuwa umbali tu wa mita kumi akishuhudia. Aliaminiwa na vijana wa
Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA
jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na
vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ameona agombee
nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara. Ingawa ni mojawapo wa
wasomi wachache kwenye jamii ya yao, ni mtu ambaye usomi wake
haujamfanya asahau mila na tamaduni za kimasai. Chakula chake, mavazi
yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni desturi za kwao na zenye
kuhuwisha Utanzania - See more at: http://salimukabunda.blogspot.com/2014/08/sokoine-is-back-in-tanzania.html#sthash.8CGC8RPc.dpuf
No comments