HAYA NDIO MANENO ALIYOSEM Robert Martinez kuhusu David Moyes.
Kocha wa Evarton Roberto Martinez amesema David Moyes
atarudisha matumaini katika maswala ya usimamizi wa mpira hivi karibuni.
Roberto
Martinez aliletwa katika klabu hiyo wakati Moyes alipoelekea
Manchester United na imesababisha timu ya Everton kuwa na ndoto za
kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa michezo yao mitatu ya msimu
iliyobaki.
Baadhi
ya mashabiki wa Everton wamemgeuka meneja wao wa zamani, ambaye
alitumia miaka 11 na klabu hiyo na kuifanikisha kumaliza katika nafasi
nne za juu mwaka 2005.
Lakini
Martinez alisema: "Tunamtakia mafanikio bora, daima tuko pamoja naye
kimawazo na sisi siku zote tunamshukuru kwa kazi aliyofanya katika klabu
yetu".
"Ni si hali nzuri kwa meneja kupoteza kazi yake, hasa mtu ambaye aliiweka katika nafasi nzuri , na nguvu klabu yetu".
"Nina
uhakika atakuwa tayari kupata kazi nyingine kwa haraka kama itawezekana
na nina uhakika yeye hakuwa mkosefu kutoa fursa kwa mtu ambaye
anafanya kazi ngumu, ana umakini na anajitolea katika kazi yake"
No comments