Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Mzungu wa Yanga aikubali Azam FC.

Mzungu wa Yanga aikubali Azam FC.

 

 Watoto wa Bakhresa hao walifunga mjadala baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 na kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

AZAM FC imemaliza mbio kali za kuwania ubingwa kwa kufanya kweli Jumapili, sasa ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara. Yanga ilikuwa ikiifukuzia timu hiyo lakini imezidiwa kete na kocha wake,
Hans Pluijm, amekubali yaishe na kukiri Azam kiboko.
Watoto wa Bakhresa hao walifunga mjadala baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 na kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm alisema walikuwa katika mbio za kuifukuzia Azam wakisubiri ipoteze mchezo wowote, lakini jambo hilo limeshindikana hivyo hana budi kumpongeza kocha wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog, pamoja na kikosi chake kwa mafanikio hayo.
“Hakuna namna nyingine zaidi ya kuipongeza Azam, wamekuwa ni washindani wazuri, tulikuwa nyuma yao tukiwafukuzia kwa karibu lakini tumeshindwa kuwapiku. Nawapa hongea,” alisema Pluijm.
“Kazi yetu kubwa sasa ni kushinda mchezo ujao ambao ushindi wake utakuwa na maana moja ya kuwafariji mashabiki wetu ambao walikuwa nyuma yetu kwa kusafiri kila tulipokuwa tunakwenda.”
Katika mechi hiyo ya mwisho ya Jumamosi, Yanga, itavaana na Simba Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa ikiwania kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 3-1 ilichokipata Desemba mwaka jana katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
Mzunguko wa kwanza, Simba ilitoka nyuma mara tatu katika matokeo ya 3-3.

 

No comments