Mgombea ubunge Kingwendu katumia dk 4 kuyasema haya ya mwisho…
Muigizaji Kingwendu ni miongoni mwa
mastaa ambao wamechukua headline za kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu
2015 kama Afande Sele, Profesa J,muigizaji Frank na wengine.
Mchekeshaji na muigizaji Kingwendu anagombea ubunge kwenye jimbo la
Kisarawe mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya CUF, Kingwendu hakuwahi
kusikika kabisa tangu kampeni zianze sasa kabla jumapili haijafika leo
amekaa na sisi kwenye exclusive na millardayo.com.
‘Tangu
kampeni zianze huku hali ni nzuri na nina faida kubwa ya kushinda sasa
hivi wazaramo wameamka wanataka mabadiliko, muda mrefu wamewapa umaskini
wamewadharirisha na wamewanyima elimu lakini mimi huku nimewafufua
vizuri wamenielewa na mikakati yangu watu wamenielewa vizuri na wako
tayari kupiga kura kwa Kingwengu’- Kingwendu
‘Nitakapo
ingia bungeni sitofanya kazi ya uchekeshaji kazi iliyonileta bungeni ni
kutetea wananchi, kuwaletea maendeleo na kufuta kero zote za wananchi si
vyema tena kuingia kwenye majukwaa na kukata viuno kwa kuwa tayari
nitakuwa mheshimiwa, Nitakapo kuwa bungeni nitaepukana na ile sauti
niliyokuwa naitumia katika sanaa nitakuwa na sauti ya kawaida nitajenga
hoja za msingi ninataka kutoa mfano kwa viongozi waliopita Kisarawe
habari ndio hiyo’- Kingwendu
No comments