Hiki ndicho kitakachofanya African Sports wasirudi Tanga kupiga kura
Licha ya kuwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limesimamisha
Ligi weekend hii kwa sababu ya kutoa fursa kwa wachezaji na mashabiki
wa soka kupata nafasi ya kupiga kura siku ya Ocober 25. Kama ambavyo
imeelezwa kuwa kila mtu anatakiwa kwenda kupiga kura katika kituo
alichojiandikishia, wachezaji wa African Sports ya Tanga hawawezi kupiga kura.
Uongozi wa African Sports kupitia kwa mwenyekiti wake Ahmed Bozinia amethibitisha kuwa hawawezi kusafirisha timu kwenda kupiga kura Tanga halafu wairudishe timu Mbeya ili icheze mechi yake na Tanzania Prisons. Afrcan Sports ilicheza mechi dhidi ya Mbeya City na kupoteza kwa goli 1-0, hivyo inasubiri kucheza mechi na Tanzania Prisons alhamisi ijayo.
“Wachezaji
wetu walijiandikisha Tanga, lakini hatuna bajeti ya kwenda Tanga kupiga
kura na kurudi Mbeya tena kwa ajili ya mechi. Tumeona ni heri kupoteza
upande mmoja kwa ajili ya maslahi ya upande mwingine. Alhamisi tuna
mchezo na Prisons jijini Mbeya City, hivyo tumeona tusubiri huku huku
ili kupunguza gharama,” >>>Ahmed Bozinia
No comments