MATUKIO NA HABARI- IDARA YA CA’s 2015 | ABDIEL SIFI
9/22/2015
MATUKIO
NA HABARI- IDARA YA CA’s 2015 | ABDIEL SIFI
|
Utangulizi:
Kanisa
Kama taasisi linapaswa kuwa na mfumo wa utunzaji kumbukumbu.Lengo ni kutunza
historia, kujipima kimaendeleo katika utendaji. Nikiwa Katibu wa idara ya
vijana kanisa la KCC nimeaona ni vema kuandika kihabari zaidi mambo machache ambayo
yametekelezwa na idara ya vijana 2015. Yaliyopo hapa ni machache kati ya mengi
yaliyofanywa na idara Pamoja na Kanisa. Nimeyachagua machache kulingana umuhimu
wake katika idara ya vijana na kanisa. Hata hivyo sisemi kuwa kila habari
itamfurahisha kila mtu, la hasha! Wengine watachukizwa. Nikiwa mwanahabari
Napenda kutoa angalizo na ulinzi wa kimaadili ya uandishi wa habari, kwamba
majina ya vyanzo vya habari ambavyo vimeshiriki kutoa maoni katika baadhi ya
mada hayajatajwa, kwa sababu ya kulinda utu, heshima zao.Izingatiwe kuwa maoni
yao si kwa nia mbaya bali ni kujenga na kurekebisha. Ukusanyanji wa maoni
umehusisha viongozi na washirika wa makanisa mabalimbali ya kiroho jijini Dar
es salaam. Nia yangu ni kuona idara ya vijana inaendeleza jarida hili la AMKA
KIJANA kila mwaka.
SHUKRANI:
Namshukuru
MUNGU kuniwezesha kufanikisha kuandika jarida hili.
·
Mama
mpendwa Mch. E. Mayala kwa ushirikiano alioutoa na kukubali kuandikwa jarida hili.
·
Dada
Janeth Kimei kwa kujitolea kuhakikisha jarida hili linachapishwa.
·
Nawashukuru
waliotoa maoni juu ya mada mbalimbali, lakini hawatataja kutokana na sababu za
kitaaluma.
MUNGU
AWABARIKI SANA.
kanisa
la KCC
Baadhi
ya vijana KCC wakifurahia jambo.
VIONGOZ I WA IDARA YA VIJANA (CA,s).
Lena
Mwavea M/kiti CA’s Yusuph
Yona Makamu M/kiti CA’s
Abdiel Sifi, Katibu CA’s.
Pendo Tarimo Mhazini CA’s
vijana wakiwa kambini Kibaha
Ijue
historia ya KCC.
Inawezekana wewe ni mshirika wa muda mrefu wa
kanisa la Kibamba Christian Center (KCC), lakini hujawahi kusikia wala kuhufahamu
historia yake. Kama yalivyo makanisa mengi kuanzia katika mazingira magumu, KCC
ni moja wapo. Chimbuko la KCC lilianza 1986 katika shule ya msingi Kibamba. Dominic Kihampa, Mwangalizi wa
Seksheni ya Kibamba na mke wake ndio walianzisha huduma shule ya msingi
Kibamba.Baada ya Mchungaji Dominic na familia yake kuhamishwa kikazi, kanisa
aliliacha kwa Mch. Moses Mayala na mke wake 1993 likiwa shule ya msingi
Kibamba. Mayala na mke wake walifanikiwa kufungua tawi Kiluvya kwa komba,
mtumishi aliyekabidhiwa kuchunga kanisa hilo aliasi hali iliyozua mgogoro kati
ya Mtumishi huyo na Kanisa la TAG. Hata hivyo kanisa hilo halikuendelea badala
yake lilibadilika na kuwa KLPT Kiluvya ambalo lipo hadi leo.Mayala aliendelea
na huduma mahali hapo hadi 1995, baada ya serikali kupiga marufuku shule za
msingi kutumika kuabudia. Mch.Mayala na mke wake walitafuta eneo jipya kwa
ajili ya kuendeleza huduma. Eneo lilipatikana mahali ambapo kanisa lipo hadi
leo.
Washirika wasiozidi 30
walianza kujenga kanisa 1993 hadi 1995 ujenzi ukakamilika na kuwekwa- jiwe la
Msingi 30, April 1995 na Askofu wa jimbo la Mashariki Magnus Mhiche. Kanisa la
KCC limefungua matawi yafutayo, Kwembe, Hondogo, Kibamba Hospitali, Kibamba
Njia Panda, Kisarawe. Waimbaji na watunzi wa Nyimbo za injili waliolelewa na
KCC ni pamoja na Ruto Rafaeli na Neema Kipangula. 2004- 2005 kanisa lillipata
Mwl, wa Kwaya Mr. Alipo ambapo kwaya ilifanikiwa kutengeneza albamu yenye
nyimbo zaidi ya 16. Albamu hiyo bado haijazinduliwa wala kurekodiwa kanda za
video kutokana na sababau mbalimbali. Kanisa hili huendesha ibada mbili kwa
lugha kiingereza na Kiswahili. KCC inaongozwa na Mchungaji Moses Mayala, Ebia
Mayala, Wachungaji wasaidizi Ibrahim Mkwiche na Isaack Kuderi. Katibu wa kanisa
akiwa Mbonea Mtaita. Pia kuna idara zifuatazo, Idara ya Maendeleo, Uinjilisti,
Maandiko, Kwaya, Sifa na Kuabudu, WWK, CMF, vjiana (CA’s), na Watoto.
Mama Mch, E.
Mayala na Mwl Methew wakiwa na
vijana katika huduma
Nini
chanzo washirika kuhama Makanisa?.
Tabia ya washirika kuhama makanisa inazidi
kukua ndani ya makanisa ya kiroho.Tabia hii isipokemewa na viongozi wa makanisa
inaweza kuleta madhara kwa kanisa la mahali pamoja.Uchunguzi wa muda mrefu
uliohusisha Wachungaji, viongozi wa idara, washirika wa makanisa mbalimbali ya
kiroho, unatoa majibu yafuatayo. Kila kanisa la mahali pamoja lina historia
yake, tangu kuanzishwa kwake, idadi ya watu walioanza huduma mahali hapo.
Lakini hao hao ambao ni waanzilishi (washirika) baadae huhamia makanisa mengine
sio kimakazi bali kusali katika makanisa hayo.Hali hii huzua maswali kwa
wachungaji washirika na viongozi wengine kwanini mtu anahama kanisa. Zipo
sababu mbalimbali ambazo husababisha mtu/watu kuhama katika hali ya
kawaida,inawezekana kuwa mtu amehamishwa kikazi hivyo analazimika kuhama mahali
anapoishi.Hapa tunazungumzia mtu ambaye hajahamishwa eneo la kazi bali anaishi
eneo lilelile lakini anahama kanisa. Maoni ya watu waliohojiwa yanajikita
katika pande mbili kama ifuatavyo. Sababu za mtu mwenyewe, pili ni mfumo wa
utawala ndani ya kanisa.
Sababu za mtu binafsi
Jada mkomba (sio jina lake), anasema “watumishi
ndani ya kanisa kutokuwa na vifua/ uwezo wa kubeba matatizo/siri za washirika, unakuta
mshirika anapitia mambo magumu na
anapomshirikisha kiongozi ndani ya kanisa, badala ya kuhifandhiwa
matatizo yake hugeuzwa kuwa mahubiri kanisani. Jambo hili linaweza kumkera mtu
kutotunziwa siri zake hivyo kuamua kuondoka”. Anaendela kusema washirika
wenyeji kutokujali washirika wapya, upendo
wa kweli kupungua miongoni mwa washirika. Matabaka ndani ya kanisa, wenye pesa
na wasio kuwa nazo. Hivyo mtu ambaye kipato chake ni kidogo anapopatwa na
matatizo ushirikiano anaoupata kutoka kwa washirika ni mdogo kuliko ule
anaoupata mtu mwenye kipato cha juu.Kibaya zaidi ni washirika kufanya dhambi ya
usengenyaji,fitina, wivu, husuda, kutetana,inachangia sana kuwaondoa watu
katika kanisa la mahali pamoja.Kinachotakiwa ni kuwasaidia na kuwaombea kwani
kwa kuwasema haiwezi kusaidia wao kuondokana na udhaifu walionao” anasema Jada.
John Nangwa (sio jina lake) ambaye ni katibu wa idara ya vijana katika kanisa fulani
Bagamoyo anasema “kitu ambacho kinasababisha watu wahame makanisa ni kuwa
na imani finyu, watu huhama makanisa
wakitafuta miujiza ya uponyaji na mafanikio bila wao kuwa na juhudi ya kuutafuta
uso wa Mungu”. Ghula Simon- anasema kanisa likiwa na viongozi wasioelewana
kutoheshimiana, uzinzi, na tabia zingine chafu husababisha kuhama kwa waumini
waaminifu na wanaopenda kuona maendeleo ya huduma yanakuwa mazuri. Maana
maendeleo hayawezi-kupatikana
kanisani ikiwa viongozi hawaelewani na kusikilizana. Kanisa likiwa na uongozi
dhaifu (wazee wa kanisa na idara) kukosa
mikakati mizuri ya kimaendeleo kiroho, huduma, kiuchumi, na kimwili kwa mtu
anayependa mambo haya yaonekene hawezi kuvumilia kuishi ndani ya kanisa kama
hilo”.kuna aina nyingine ya watu kuhama, wakati ambapo kiongozi wa juu kanisani
akihama, washirika dhaifu wa imani huunga behewa kufuatia sababu ambazo huyo kiongozi
zilisababisha yeye kuhama, hasa ikizingatiwa kuwa kiongozi huyo aliheshimika na
kupendwa kanisani anasema Ghula.
Sababu
za mfumo wa utawala
Mchungaji Kilio kalemela (sio jina lake)
anasema “Hapo zamani kulikuwa na utaratibu wa kanisa la TAG wa kupokea wageni,
ambao siku hizi hauzingatiwi sana na viongozi wa kanisa. Ilikuwa lazima mtu
anayehamia kuwa na barua ya utambulisho wa kanisa analotoka ambayo huiwasilisha
kanisa analohamia.Utaratibu huu hauzingatiwi hivyo mgeni hupokelewa bila barua,
badala yake hujieleza tu kwa viongozi wa kanisa na kupokelewa. Maelezo pekee
hayatoshi- kuaminika kwamba taarifa zake ni sahihi au la!. Lakini pia jitihada
za makusudi hazifanyiki kujua ni wapi alipotoka ili kujiridhisha. Hivyo,
akiamua kuodoka anaondoka tu! tena bila kuaga, anasema Mchungaji Kalemela.
“Tabia ya washirika kuhama makanisa inaendelea kukua na kupanuka hasa makanisa
ya mijini na isipoangaliwa kwa makini itabasabisha kanisa kutoendelea na kukua
katika huduma maana watu wamebeba huduma ambazo zingekuuzwa na kulelewa mahali
pamoja zitaimarika zaidi na kukua. Mchungaji Kilio anataja sababu nyingine kuwa
demokrasia ndani ya kanisa ni muhimu ikawepo, viongozi, washirika kuwa na uwezo
wa kuhoji, kukosoa na kutoa maoni yao juu ya mambo yanayohusu kanisa.Mgawanyo
wa majukumu lazima uzingatiwe ndani ya kanisa. Unaweza kukuta Mchungaji
Kiongozi anakuwa na majukumu mengi kupindukia hali inayosababisha kuzidiwa na kushindwa
kumudu. Usaidizi ni Mzuri kama ambavyo alifanya Musa kwa kuwateua Maliwali na
Maakida ili wamsaidie majukumu ikiwemo kusikiliza na kutatua matatizo yao.Kanisa
ni taasisi ambayo inatakiwa kuendeshwa kiitifaki/kila kiongozi awe na mamlaka
ya kusimamia majukumu yake bila kuingiliwa.Wachungaji kuwa waamuzi wa kila
jambo unafanya viongozi wengine wa idara kumtegema mchungaji.Hii inasababisha
viongozi wa idara kutojitegemea kimaamuzi katika nafasi zao” anasema.
Sababu nyingine ni kutojali watu
wenye huduma au wito maalum. “Mungu ametupa vipawa na uwezo tofauti kila mmoja,
inapotokea mtu anahamia ndani ya kanisa akiwa na wito katika huduma fulani
hukosa nafasi ya kufanya huduma hiyo. Ikihofiwa kwamba anaweza kuwakosesha
nafasi waliokuwepo kuhudumu. Mtu wa namna hiyo kwa kuwa anajua kumtumikia Mungu
katika huduma yake hawezi kuendelea kudidimiza huduma hiyo bali atatafuta
sehemu ambayo anaweza kutumika”.Washirika hupatikana kanisani kwa njia mbili
kuu,ushuhudiaji na kuhamia. Hivyo kanisa lina wajibu wa kuhakikisha lina kuwa
na utaratibu wa kuwachunga watu wake, kuwasilikiza pamoja na kuwafundisha huduma na kutumika.Hii
itasababisha mtu kuwa na imani ya kweli
na Mungu anayemwabudu na kubaki kanisani na sio kutanga tanga akitafuata
Miujiza. Akinukuu biblia Takatifu “Mithali 14: 28 (utukufu wa mfalme ni wingi
wa watu wake, bali uchache wa watu ni uharibifu kwa mkuu wao )” Hivyo
kanisa linapokuwa na watu wengi maana yake ni Utukufu kwa Mungu na Mchungaji.
Mungu anapenda watu wakusanyike kwa wingi wamwabudu na kumsifu yeye katika roho
na kweli, kinyume chake ni uharibifu.
Nini kifanyike.
Kutokana na
changamoto hizi zinazokabili makanisa ya kiroho, kunahitajika mambo kadhaa
kuzingatiwa ili kuondoa tabia ya watu kuhama makanisa badala yake wakuuzwe
kulelewa na- kuendelezwa kwa huduma zao ili kuleta mandeleo ya kiroho na
kimwili ndani ya kanisa.Kwanza kabisa ni lazima kanisa liwe na mfumo wa kisasa
wa kupokea wageni na kuwalea vizuri,Wachungaji, wazee wa kanisa na Wakuu wa
idara washirikiane kuhakikisha wageni wanalelewa vizuri na kukuzwa kiroho.Kuwajali
washirika na kudumisha upendo, kusikiliza mahitaji na kuwatunzia siri na
matatizo yao. Kuwa na uongozi thabiti unaojikita katika mipango mikakati mizuri
ya kukuza huduma na kuondoa matabaka ndani ya kanisa, kwamba wenye pesa na
wasio kuwa nazo wawe kitu kimoja katika mwili wa Kristo ili kuleta uhai wa
huduma iliyosimama imara. Kwa kufanya hivyo kanisa litakuwa kama taa
inayoangaza gizani na kuwavuta watu.
Mchungaji awataka vijana kuacha uzembe.
Mchungaji Msaidizi Pasco Masawii wa kanisa la TAG Maili Moja
amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha uzembe ili waweze kujikwamua
kiuchumi. Alisema hayo wakati akifundisha vijana katika kambi ya wiki moja ya
vijana iliyoshirikisha vijana 104 kutoka seksheni ya Mbezi na Kibamba
iliyofanyika Wilayani Kibaha kuanzia Julai 22-27 2015.“Inashangaza kuona vijana
waliookoka wamebweteka tu, -hawajishughulishi na kazi hali inayosababisha kuwa
nyuma kimaendeleo ya kiroho na kimwili.Watu wanaopenda kupata kirahisi, wavivu
na wenye aibu ya kufanya kazi.Tabia hii ndio chanzo cha kudhaulika katika jamii
na kwamba hata wokovu wao hutiliwa mashaka.”[i]Mchungaji Masawii aliwaeleza vijana kuwa wanapaswa
kufanya kazi kwa bidii, ili kujijengea sifa njema na kwamba inapofika wakati wa
kuoa au kuolewa ni rahisi kwa sababu msichana / mvulana hupenda kuoa / kuolewa
na mtu mchapa kazi, mwenye hofu ya Mungu. Akitolea mfano kijana Simon Mwashiuya
kutoka TAG Kibamba (KCC) ambaye alifika kambini akiwa na karanga kwa ajili ya
biashara, kuwa ni kijana anayejituma na kujishughulisha hivyo Mungu lazima
atamwinua.Mchungaji Masawii aliitisha changizo kwa ajili ya kumwongezea mtaji
ambapo zaidi elfu 50,000 zilipatikana. Pamoja na hayo Mchungaji aliwaonya
vijana wote kujiepusha na vitendo viovu badala yake wamtumikie Mungu kwa
uaminifu.
_________________________________________
Badiliko la kiroho
huleta haki Kwa Taifa.
Kwa upande mmoja (ukizingatia utawala wa Warumi) kuna wanaotoa maoni kwamba
Yesu wa Nazareti alikuwa na makosa.Kwamba alijiita- masiha na alikuwa na-
mpango wa kuupindua utawala wa Warumi. Wanasema Yesu wa Nazareti, alianzisha
vuguvugu la kisiasa na kidini (Religion-political movement).Kwamba hata yeye
hakuwa tofauti na makundi mengine yaliyokuwa yakipigania Uhuru wa Israeli, kama
vile Zealots na wengine.Kati ya wafuasi wake walitoka kwenye makundi haya ya
wapigania uhuru: “Matayo na Toma, Yakobo na Alfayo na Simoni (aliyeitwa
Zeloti), Yuda Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa mhaini” (Luka
6:15-16).Kwamba yeye alisisitiza ufalme wa kiroho. Ya Kaizari yaende kwa Kaisari
na ya Mungu yaende kwa Mungu. Kwamba- mafundisho yake yote yalikuwa ni ya
kiroho. Mashtaka ya kisiasa juu yake yalipikwa na viongozi wa Wayahudi
waliomchukia. Hata hivyo, Ukweli juu ya Yesu wa Nazareti, haukujikita kwenye
maoni ya pande hizi tofauti. Pia, kuna ukweli kwamba Wayahudi hawakutofautisha
siasa na dini.Kile ambacho leo tunakiita siasa, masuala ya kijamii, uchumi na
dini, kwao ilijulikana kama Mungu na sheria. Hakuna kitu chochote katika jamii
ile ya Wayahudi kilichojitegemea bila kuegemea kwa Mungu na sheria.Mungu,
aliyaongoza maisha yao, aliwalisha, aliwanywesha, aliwalaza na kuwaamsha,
aliwaelekeza la kufanya na kuacha, aliwahamisha kutoka nchi hadi nyingine na
mwishowe aliwapatia nchi nzuri yenye maziwa na asali! Alikuwa Mungu wa wivu!. Hakutaka
wawe na uhusiano na miungu wengi, au wafanye mambo yasiyompendeza. Hivyo siasa
kama siasa tunavyoifahamu leo hii haikuwepo katika maisha ya jamii ya Wayahudi.
Ndiyo maana walipigana kufa na kupona kuondoa utawala wa Warumi uliokuwa
ukitenga siasa na dini. Yesu wa Nazareti, alitaka kuikomboa Israeli kutokana na
utawala unaotenga dini na siasa. Lakini yeye alikuwa na maoni tofauti na
wengine. Yeye aliamini kwamba- ukombozi huu ungewezekana kama Israeli
ingebadilika kutoka rohoni. Ni lazima kubadilika kutenda wema, haki na huruma.
Bila hivyo hata kama wangefanikiwa kuwapindua na kuwafukuza Warumi, watawala wa
Kiyahudi wasingekuwa tofauti.Yesu wa Nazareti alionyesha waziwazi kwamba maisha
ya kitabaka yaliyokuwa miongoni mwa jamii ya Wayahudi yalikuwa ni ya
kiunyanyasaji zaidi ya utawala wa Kirumi. Hivyo la msingi siyo kubadilisha
utawala, bali ni kubadilisha roho za watu, bila kufanya hivyo hakuna ukombozi
wa kweli!. Hapa ndipo kuna somo hata kwetu sisi hapa Tanzania. Watu na
wanasiasa wamekuwa na hamu na shauku ya kubadilisha utawala kutoka CCM na
kwenda kwa vyama vingine ili kuleta mabadiliko katika utendaji na kupambana na
rushwa na ufisadi.Maaskofu wetu wanafikiri elimu ya uraia inaweza kusaidia
kupambana na rushwa na ufisadi. Kama ilivyokuwa wakati wa Yesu, hata sisi
mabadiliko yetu hayawezi kuleta matunda mema, kama hakuna mabadiliko kutoka
rohoni. Ni lazima kwanza Tanzania, ibadilike kutoka rohoni. Ijenge kwanza mifumo
ya kuhimiza matendo ya wema, haki na huruma. Kinyume na hapo, hata vyama
vingine vitatenda kama ilivyokuwa ikitenda CCM! Wale wote wanaolilia mabadiliko
ni lazima walifahamu hili kwanza ndipo tusonge mbele. Vinginevyo tutabaki
palepale!.Utawala wa Kirumi, ulimaanisha kulipa kodi ya Kirumi; kama ulivyo
utawala wowote hapa duniani. Kodi ni kitu kinachotangulizwa!.Kwa Wayahudi
kulipa kodi kwa Warumi kulimaanisha kumpatia Kaizari vilivyo vya Mungu: Yaani
Israeli na mali zake zote. Yesu alikuwa na maoni tofauti: “Basi, baadhi ya
Wafarisayo na Waherodi walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake. Wakamwendea,
wakamwambia, ‘Mwalimu, tunafahamu kwamba wewe ni mtu anayesema ukweli mtupu,
wala humjali mtu ye yote. Wala hujali cheo cha mtu lakini huwafundisha ukweli
kuhusu njia ya Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaiaziri au la! Tulipe au
tusilipe’? Lakini Yesu akijua unafiki wao akawaambia, ‘Mbona mnanijaribu?
Nionyesheni sarafu’ Wakamwonyesha.Naye akawauliza, ‘Picha na chapa hii ni vya
nani?’ Wakajibu, ‘Ni vya Kaisari’. Basi, Yesu akawaambia, ‘Mpeni Kaisari
vilivyo vyake Kaisari na Mungu vilivyo vyake Mungu”...(Marko 12: 1-17).Fedha
zilikuwa na picha ya Kaisari, hivyo kukataa kumpatia kodi Kaisari ni ishara ya
kupenda fedha na mali. Ili kumpatia Mungu, vilivyo vya Mungu ni kuuza vitu
vyote na kuwapatia fedha maskini, ni kuachana na tamaa ya kupenda madaraka na
kuishi kwa anasa. Somo hapa ni kwamba Kwa Mungu, hakuna fedha, kwa Mungu,
hakuna kuuza na kununua. Kwa Mungu kuna kupewa bure na kutoa bure.Hiyo ndiyo
changamoto ya maisha ambayo hadi leo hii iko mbele yetu. Kuuza na kununua siyo
utamaduni wa wale wanaomfuata Yesu wa Nazareti.Utamaduni wao, ambao ulijengwa
na mwanzilishi wa- imani hii, ni kutoa bure, maana tunapokea bure kutoka kwa
Mwenyezi Mungu. Pia, utamaduni wa kuuza na kununua siyo wa Mungu. Sote,
tunapokea vipaji, tunapokea maisha bure kutoka kwa Mwenyezi Mungu – hakuna
anayelipa chochote ili kuupata uhai, hakuna anayelipa chochote ili kupata
vipaji, akili, hekima na busara.Yote tunapewa bure na tunaagizwa kutoa bure!
Bila kutenga dini na siasa, jambo hili linawezekana! Mungu, akiwa kiongozi wetu
– na siasa zote zikachipuka kutoka kwa Mungu tunaweza kuendeleza sera
ya:“Tumepewa bure na tutoe bure” – sera ambayo inaweza kujenga amani ya kudumu
hapa duniani. Vita na mapambano yote tunayoyashuhudia hivi leo ni kwa sababu
dunia ilijiingiza kwenye mfumo wa kuuza na kununua.Jambo hili linaitesa dunia
na litaendelea kuitesa, hadi pale tutakapotambua mafundisho ya Bwana Yesu wa
Nazareti ya kupewa bure na kutoa bure,Wenye vingi, wanataka kuwauzia wenye
vichache, lakini siyo kuwauzia bali kutaka kuwatawala kimawazo na
kiuchumi.Mungu. Hapo ndipo mapambano yanaanza, maana kila mtu ameumbwa na uhuru
wake na daima kuna kishawishi cha kutetea uhuru huu. Inawezekana wengine wakapigana
na kuupata uhuru, lakini bila mabadiliko ya rohoni, uhuru wao unakuwa hauna
maana yoyote, hata wanaopata uhuru wao, wanaendelea kunyanyasana wao kwa wao.
Hoja ya msingi aliyoishughulikia Yesu wa Nazareti ni unyanyasaji, siyo kwamba
wakoloni Warumi waliitawala Israeli. Yeye aliguswa na unyanyasaji uliokuwa
ukiendelea miongoni mwa jamii ya Wayahudi. Aliguswa na umaskini, magonjwa, njaa
na ubaguzi wa kupindukia. Hakuangalia kama anayesababisha yote hayo ni Mkoloni
Mrumi au Myahudi. Aliuchukia uovu! Jamii yoyote ile ikiwa na utamaduni wa
unyanyasaji na ubaguzi, hata kama si ya kikoloni – haimpendezi Mwenyezi
Mungu.Wale waliopinga utawala wa Warumi na kuendeleza unyanyasaji na ubaguzi
miongoni mwa jamii ya Wayahudi hawakuwa na tofauti na wakoloni Warumi. Hivyo,
Yesu alibadilisha mwelekeo wa mapambano kutoka kupinga utawala wa Warumi na
kuelekeza mapambano kwenye kutetea maskini na wenye dhambi. Huu ni msimamo
tofauti na wa wale waliokuwa wanapigania utaifa wa Israeli, upekee wa Wayahudi,
upekee wa dini ya Wayahudi, ubora wa Wayahudi na kwamba wao ni taifa teule. Huu
haukuwa msimamo wa ukombozi wa kweli. Ukombozi wa kweli, kama alivyoonyesha
Yesu wa Nazareti, ni kuuthamini ubinadamu. Kumpenda adui ni msimamo wa
kuthamini mshikamano wa binadamu wote.
Makala
hayo hapo juu yamenyofolewa kutoka tovuti ya www.mwananchi.co.tz yaliyoandikwa na Privatus Karugendo Machi
2015.yamewekwa hapa kutoka na umuhimu wake kiroho
Mch. Mkwiche: Tunapaswa kuombea Taifa letu.
“Kwa
kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2015, tumeshudia Taifa letu likikabiliwa na
matatizo mengi ambayo yanatukumbusha wajibu wetu wa kumwomba Mungu haya
ayasiendelee kutokea” ni maneno ya Mchungaji- msaidizi Ibrahim Mkwiche wa
Kanisa la Kibamba Christian Center (KCC). Akiyataja baadhi ya matatizo
yanayoendelea kulitesa Taifa, ni kuongezeka kwa ajali za barabarani, mauaji ya
albino, na utekaji wa watoto.“ Ajali iiyotokea mkoani Njombe iliyohusisha basi
la Majinjah kugongana na lori la mizigo iliua zaidi ya watu 50, ajali zingine
mbili zilizotokea mkoani Morogoro, ziliangamiza watu zaidi ya 20, kufungiwa kwa
watoto 18 wilayani Moshi na mauaji ya Albino yanayoendelea katika sehemu
mbalimbali nchini, yanaashiria ni namna gani watu wamekuwa wakatili waovu na
waonevu, hali hii haivumiliki kwa Mungu hata Kidogo.Tunao wajibu kama watu-
wanaomwamini Mungu na wenye mapenzi mena na nchi yetu, hivyo tunapaswa
kuliombea Taifa letu ili Mungu aepushe haya yasiendelee kutokea” alisema.Ikiwa
watu wanaomwamini Mungu hawatachukua hatua stahiki kwa kuliombea Taifa basi ni
Vigumu Mungu kuiponya na akuibariki nchi kama ailivyoandikwa katika biblia 2Nyakati7:14 ikiwa
watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha na- kuomba na kuutaafuta
uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kusamehe nchi
yao na kuiponya nchi yao.Katika hali ya kawaida lazima tujiulize kama
Taifa, kama waumini na kama wananchi kwanini haya yanatokea.Ndugu zetu wanauawa
kwa imani za kishirikina,wengine wanapoteza maisha kwa ajali,kukithiri kwa
vitendo vya kikatili na viovu, bila shaka ni kwa sababu tunamkosea Mungu na hivyo anatupa onyo ili tumrudie
yeye. Kwa maana hiyo hawezi kuibariki nchi na watu wake ikiwa hawajajisahihisha
kwanza. Hata hivyo aliwaomba washirika kuomba Mungu kwa bidii sana wakati huu
Nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu ili kupata viongozi ambao watafaa na
kuongoza Taifa katika misingi ya haki na usawa.
_________________________________________
Hongera
Mchungaji Moses Mayala.
Katika kuhakikisha kuwa huduma ndani ya kanisa
TAG Kibamba zinapanuka Mchungaji Kiongozi Moses Mayala alianzisha ibada kwa
lugha mbili tofauti Ibada ya kwanza kwa lugha ya kiingereza ambayo huanza Saa
1:00 kila jumapili ikiwalenga watu wanaopendelea kupokea neno la Mungu kwa
Lugha hiyo. Pia ibada ya Kiswahili ambayo huanza saa 4:00 asubuhi kila-
jumapili.Kuwepo Kwa ibada hizi mbili kwa lugha tofauti kumetoa uhuru wa watu
kuabudu kwa lugha anayoipenda.
Katika kuhakikisha vijana wanakua katika huduma
kanisani Mchungaji ametoa nafasi pana kwa vijana kuhudumu katika ibada
hizi.Hata hivyo ibada zote hizi zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinahitaji kuepukwa mara moja. Moja na kubwa ni washirika kuchelewa ibadani
hali ambayo inasababisha ratiba za ibada kutofuatwa kama inavyotakiwa.
__________________________________________
CA’s ya KCC yang’ara.
Mwanzoni
mwa mwaka huu, viongozi wa kanisa kushirikiana na idara zote kanisani
wamewezesha vijana kushiriki katika mikutano na semina mbalimbali
zilizoandaliwa nje na ndani ya kanisa, Seksheni, na Jimbo. Katika semina ya
wiki moja iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu kanisani iliyoshirikisha vijana
zaidi ya 50 ambapo walifundishwa masomo kama mahusiano, uchumba na ndoa na
maadili ya kijana aliyeokoka. Mwalimu aliyesimamia semina hiyo Mama Methew
alikiri kufurahishwa na ushiriki wa vijana katika
semina
hiyo.Mwezi July vijana nane walishiriki katika kambi ya Seksheni ya Kibamba na
Mbezi iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mwenyekiti wa vijana Lena Mwavea
amekuwa mstari wa mbele amasisha vijana kushiriki fursa mabalilmbali kujifunza
neno, huduma na kumtumikia Mungu, ambaye pia alikuwemo katika kambi hiyo.
Wengine waliohudhuria ni Katibu wa vijana Abdiel Sifi, Mhazini wa idara Pendo
Tarimo, Mpiga gitaa maarufu Jeremiah Mayala, David Traifon, Emanuel Mbwambo,
Salome Mayala na Simon Mwashiuya. Hata
hivyo vijana wa KCC waliibuka vinara katika kambi hiyo baada ya kuonesha uwezo
katika mambo tofauti, Emmanuel Mbwambo alionesha umahiri mkubwa katika utunzi
wa igizo ambalo lilichukua nafasi ya kwanza. Naye katibu wa vijana Abdiel Sifi
alionesha kipaji cha Utangazaji baada ya kutangaza habari zote zilizotokea
katika kambi hiyo. Kubwa zaidi ni baada ya
Simon Mwashiuya kunyookewa na mkono wa Mungu na kukusanya zaidi ya elfu
50 kuongezea mtaji wa biashara yake ya karanga.Idara hiyo pia imeshiriki
matukio makubwa ya kitaifa ambapo mwezi Agosti Vijana waliaonesha moyo wa
kumpenda Mungu kwa kuchangia zaidi ya shilingi 100,000 ili kumuewezesha kiongozi
mmoja awakilishe idara katika mkutano wa
vijana kitaifa uliofanyika Mjini Dodoma. Jimbo la Mashariki kaskazini lilishika
namba moja katika majimbo yaliyopeleka wajumbe wengi zaidi. Nafasi ya kwanza
ikishikiliwa na Jimbo la Mashariki Kusini.
___________________________________________
Hitimisho
Napenda
kumshukushuru Mch.Moses Mayala, Ebia Mayala na viongozi wote wa idara zote
kwa kazi kubwa wanayofanya kutulea
vijana na kanisa.
Shukrani
kwa timu ya sifa na kuabudu (praise & worship team) chini ya Daniel Mayala
kwa bidii kubwa ya kumtumkia Mungu.
Washirika
wote kwa umoja wao.
Zaidi ya
yote kama kanisa tudumu katika upendo na tusikate tamaa pia kuonyanyana katika
jina la Yesu.
Upendo na udumu katika ndugu:
Ebr . 13:1
No comments