Tamko jipya la madereva baada ya mwenzao kupigwa risasi kisa laki 4…(Pichaz)
Matukio ya watu kupigwa risasi yamekuwa
yakichukuwa headlines kubwa hasa kwa Dar es salaam lakini sio mwajiri
kumpiga risasi mfanyakazi wake, Sasa hii imekuwa tofauti kidogo ambapo
Jumanne ya wiki hii ililipotiwa tukio la Mwajiri kumpiga risasi
mfanyakazi wake baada ya kusababishia Kampuni ya Tripple A KTM, hasara
ya dola za Kimarekani 200 sawa na 400,000 za kitanzania na lita 700 za
mafuta baada ya kufika nchini akitokea Congo.
Akiongea na ripota wa millardayo.com Naibu katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa madereva (TADWU) Rashidi Salehe…’Niliongea
na marehemu nusu saa kabla ya kifo chake akinitaarifu kuwa anashoti ya
lita sabini za mafuta na anaupungufu wa dola mia mbili (200) ambazo
alizitoa kama sehemu ya faini ya mizani upande wa Zambia sehemu ya
Kapilimposhi, kwahiyo alikuwa akinitaarifu huwenda anaweza akapelekwa
Chang’ombe kituo cha Polisi ambacho amekuwa akikitumia sana mmiliki
kuwapeleka madereva akanimbia kwamba niwe na angalizo huwenda akawekwa
ndani,dakika kumi baadae nilipigiawa simu na mwanachama wetu mbaye ni
deverva wa kampuni hiyo kwamba David amepigwa risasi na ameanguka
chini’>>>Rashidi Salehe Naibu Katibu TADWU
‘Sasa
leo tunataka kuona kupitia kilio chetu cha kudai maslahi yetu na
hatimaye mauaji serikali inatoa tamko gani? lakini sisi kama vyama vya
wafanyakazi tumelaani tukio hili na tunasema kwamba hatua zichukuliwe
haraka iwezekanavyo, tumejitahidi sana kuwatuliza madreva watulie katika
kipindi hiki vinginevyo hatua ilikuwa mbaya zaidi juu ya magari ya
mmiliki huyo yaliyokuwa boda na Dar es salaamu kwa sababu amekuwa
akiyafanya mambo haya marakwamara suala la kupiga bastola kupiga mpaka
ilifikia hatua Kova alidhibitisha kwamba bastola yake ilikamatwa kwa
mara ya kwanza’>>> Rashidi – TADWU
‘Endapo
kesi hii itasimama maahakamani kila siku ya mahakama tutakuwa
tunasitisha usafiri nchi nzima kama sehemu ya kilio chetu juu ya mauaji
ya kinyama yaliofanyika kwa dereva mwenzetu Bwana David
Kilangula’>>>Rashidi- TADWU
Source: Millard Ayo
No comments