HEKAHEKA: Baada ya ‘Scorpion’, hii nyingine imetokea DSM ya Rambo mkata mapanga
Wiki
chache baada ya kutokea kwa stori za ‘Scorpion’ ambaye alizichukua
headlines kutokana na kuhusishwa kwake na matukio ya uporaji na
kuwadhuru watu kadhaa kwenye maeneo ya Buguruni Jijini Dar es salaam,
Leo Heka Heka ya Clouds FM imekuja na stori nyingine ya Rambo mkata
mapanga.
Geah Habib
kupitia Leo Tena ameipata stori hii ya jamaa anayefahamika kwa jina la
Rambo kutoka maeneo ya Karakata, Uwanja wa Ndege Dar es salaam. Huyu
jamaa inadaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwapora watu na wengine
kuwakata mapanga.
Wananchi
wa maeneo hayo wamezungumzia vitisho ambavyo wamekuwa wakivipata kutoka
kwa Rambo ambaye aliwahi kufungwa jela na kuachiwa wiki mbili mpaka tatu
zilizopita. Wanawake wengi wameonesha kumuogopa Rambo kwa madai kwamba
anaweza kuwadhuru kwasababu hata wanaume zao wamekuwa wakihofia kurudi
nyumbani inapotokea wamechelewa kurudi au wanarudi mapema ili kumkwepa.
>>>’Yule
mtu alifanya fujo mtaani akakamatwa, tangu kipindi cha Kova, walimweka
ndani lakini wamemuachia tena amerudi kutunyanyasa tena wananchi. Sisi
tunailaumu serikali kwanini wamemuachia, mtu amechoma watu visu, amekata
wanawake matiti, wanaume wenyewe wanamuogopa’- Mwananchi
>>>’Huyu
Rambo ni shida na alianza haya mambo kitambo kidogo alikuwa anakata
watu mapanga kweli alikamatwa na polisi akapelekwa mahakamani
akahukumiwa kifungo. Lakini baadaye walikata rufaa akatolewa jela. Baada
ya kutoka jela akavamia watu akawakata mapanga watu eneo la shule ya
msingi Muhogo akachukua simu akaondoka nayo’ – Diwani wa Sitaki Shari. zaidi bofya hii link: http://millardayo.com/0hekaheka8/
No comments