Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Yanga imeitoa Cercle de Jochim ya Mauritius, sasa itakutana na timu hii

February 27 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilishuka dimbani kumenyana na klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika mchezo wake wa pili wa hatua ya kwanza ya michuano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Yanga walikuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea na hatua inayofuata, baada ya mchezo wa kwanza waliocheza Mauritius kuibuka na ushindi wa goli 1-0, hivyo Cercle de Joachim walikuja kwa nia ya kupata ushindi ili waendelea hatua inayofuata.
DSC_0771
Hata hivyo hali haikuwa rahisi kwa Cercle de Joachim kupata matokeo katika mchezo huo, kwani dakika ya 3 Yanga walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Amissi Tambwe, goli la pili la Yanga lilifungwa na Thabani Kamusoko dakika ya 55 baada ya kutumia vyema mpira wa faulo.
DSC_0770
Licha ya kumkosa Donald Ngoma katika mchezo huo, Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, hivyo watacheza na APR ya Rwanda katika hatua inayofuata na itaanzia kucheza ugenini mjini Kigali  mwanzoni mwa mwezi March, na baada ya wiki mbili kurudiana uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
source: Millard Ayo.

No comments