Tehama inakuza au inadumaza fikra kwa watoto?
Tehama inakuza au inadumaza fikra kwa
watoto?
Na Abdiel Sifi
"Mapinduzi yanaletwa na watu, watu wanaofikiri kama watu wa vitendo na
kutenda kama watu wenye fikra” aliwahi kusema Rais wa Ghana Nkwame Nkuruma wakati wa uhai wake.
Maendeleo Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) yamechukua nafasi kubwa katika maisha ya Watanzania.Fikira
zetu zote tumezielekeza katika ombwe la
Teknolojia hii.
Ni wakati ambapo binadamu hasa Waafrika kama sio Watanzania tumebaki kuwa watumiaji
wa nyezo hizi za mawasiliano pasina kuangalia kwa makini jinsi zinavyodhoofisha
uwezo wa fikra zetu.
Hali ni mbaya zaidi kwa watoto wanaozaliwa karne hii ya 21,ni waathirika
wakubwa wa maendeeleo haya. Wazazi hupenda kuwafurahisha na kuwaburudisha watoto
wao, huwanunulia zawadi, kama mwanasesere (mdoli) bunduki na ndege za plastiki,magari,baiskeli,
simu zenye michezo au muziki nk.
Muda wote mtoto akiwa nyumbani hujishughulisha na madubwasha haya, anajifanya
anapiga risasi, anaendesha gari, kucheza michezo ya komputa, simu nk.
Michezo ya siku nzima mtoto hushinda akijifariji na midoli, ‘gemu’ gari
baiskeli nk.. Sisemi kwamba hayafai, la hasha! Ni mazuri lakini swali la
kujiuliza ni nchi gani Duniani iliyopata maendeleo kwa kutumia zana,fikira,
utamaduni wa Taifa lingine? Hapa kidogo nigusie mambo ya asili yanayopambanua jamii moja na nyingine, Lugha ubunifu, utamaduni nk.
Ikiwa mtoto huyu hushinda kutwa kwa kubinyabinya bunduki ya kichina na
kucheza michezo ya komputa , nafasi yake ya ubinifu itatoka wapi? Utamaduni
wake ni upi?
Historia inaonesha kabla ya wazungu kuvamia bara la giza, waafrika walikuwa
na ubunifu wa asili.Walitengeneza vifaa walivyovitumia katika maisha yao, kama
mkeka, kuchonga viti, mizinga,uvuvi, kilimo, kutengeneza nguo kwa kutumia ngozi
za wanyama na magome ya miti nk, swali
la kujiuliza ni nani aliwafundisha haya?
Walijipambanua hivyo kulingana na mazingira ya maisha yao, baadaye jamii
ilipitia mabadiliko mbalimbali ya kimaendelao mpaka wakati huu. Baada ya uhuru
Serikali ilianzisha sera ya elimu ya
kujitegemea na ujamaa.Ilihimiza juu ya kutafuta,kuthamini, maarifa na elimu ili
mtu aweze kujitegemea,kuwa huru katika uamuzi wa mambo yake mwenyewe.
Lengo lingine lilikuwa ni Kumwezesha mwanafunzi kujivunia utaifa na
utamaduni wa Taifa la Tanzania. Elimu hii ilimtaka kijana kudumisha mila na
desturi za kitanzania na kuachana na mila za kigeni ambazo zilionekana kuharibu
utaifa wa Tanzania.
Hivyo basi kwa kuwa tunafikiri kuwa watoto wetu watapata elimu na maarifa
kwa kutukuza vitu vinavyoletwa na wazungu kama ishara ya kuwaburudisha kumbe ni
kuwangamiza katika fikira na hivyo
tusitarajie mabadiliko katika maisha yao baadaye.
Zamani watoto walijifunza vitu vingi utotoni na vilikangaza akili na mwili,
hasa panapochagiza na kufundishwa na
mzazi.
Kwa mazingira ya usasa ambao uliopo , watoto wetu Leo, hawawezi kuumba,
kuunda na kujishughulisha na fikira zaidi ya kutegemea vya wazungu.
Hawajiamini, magoigoi, mbumbumbu hali inayosababisha kumaliza darasa la saba mtu hajui hata kusoma.
Wanapofikia umri wa ujana watoto wanakumbana na janga lingine, amabalo
linaua na kumaliza kabisa fikira zao. Si mtoto tena, yupo kidato cha tatu au
nne. Mazingira yanayomzunguka ya kutokuwa na fikira na kutukuza ya wazungu naye
huingia mzima mzima.
Kijana wa kisasa, ana simu kali, yenye programu kama facebook, twitter,
instagram whats app nk.Akili na fahamu zao zimejengeka katika matumizi ya
mitandao ya kijmii.
Vijana wa vyuo Sekondari na watu wengine utawaona wamebeba
simu kubwa mikononi. Kazi ni kupapasa
vioo vya simu zao.ukidhani wanatafuta maarifa na kujifunza mambo ya msingi
unakosea! ni kusifu picha za nusu uchi wanazoweka dada zetu wazuri wa Tanzania .
Tabia hii ya kusifu picha za wasichana Mitandaoni, imetawala fikira za
vijana kwa leo. Mtu anaamka asubuhi anatafuta, nyumba, jengo, au gari na alafu
apige picha halafu anaiweka mtandaoni ili watu waisifu.
Wasichana wameenda mbali zaidi, wanapiga picha zinazoonesha viungo vyao,kisha
kuweka mtandaoni ili watu waisifu picha
yake.Kwa sababu watu walio katika mkondo huu ni wajinga, bila hiyana huisifu
picha kwa maneno ya manukato. Inawezekanaje kuisifu picha ya mwanamke aliye
nusu uchi,au aliyepiga picha akiwa ndani ya gari ilihali hata kupiga honi
hajui?. Ni kupoteza muda bila faida.
Walimu shuleni wanapiga kelele,marufuku mwanafunzi kuwa na simu shuleni. Kwa
kuwa wamejawa na ujinga hupingna na utaratibu huo. Mwishowe huishia kufukuzwa
shule. Kumzuia mwanafunzi kutokuwa na simu Shuleni ni jambo la maana sana.Kumfanya
mwanafunzi aweke bidii katika jambo moja tu, kusoma.
Ikiwa jamii yetu itaathiriwa hasi zaidi , hatari iliyopo ni kuwa naTaifa la
watu wajinga wasiofikiri kama watu wenye fikira. Sisemi njia hizi ni mbaya la
hasha! Tunazitumia kinyume. Kujidhalilisha, kuudhalilisha utu wake, hivyo
hatufikiri kama watu wenye fikira kama alivyosema Nkuruma miaka mingi iliyopita
Azimio la Arusha 1967 kuna
kipengele kinachosema “Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara kanuni
za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu” ikiwa mtu kwa utashi wake anaweka picha
ya uchi mtandaoni maana yake
ameshindwa kujiheshimu na hivyo
anajidhalilisha yeye, utu wake, na jamii yake ambayo haina utamaduni wa namna
hiyo.
Ameshindwa kuheshimu haki yake
kama binadamu,hii si tabia nzuri ya kuvumilika.
Ndio maana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha mswada
wa sheria ya makosa mtandaoni ambao unasubiriwa kusainiwa na Rais na kuwa
sheria. Ikiwa mswada huo utasainiwa basi kutakuwa na sheria itakayoweza kuzuia
matumizi hasi ya mitandao ya kijamii.
Mwalimu nyerere alisizitiza kuwa
ili watu waendelee ni lazima kuweka bidii kuondoa ujinga na kujijengea
uwezo,elimu,na ufahamu wa kukabilina na changamoto za maisha.kuhakikisha hilo
linafanikiwa serikali iliweka juhudi kuchapisha vitabu, kujenga shule na
kuanzisha taasisi mbalimbali za elimu kama elimu ya watu wazima lengo likiwa
kuleta mapainduzi ya fikira kwa binadamu , kupanua, kukabiliana na kutatua
matatizo ya kisiasa kiutawala na kijamii.
Bado tuna maduka machache sana ya vitabu;hatuna utamaduni wa kununua
vitabu; halafu usomaji wetu unazidi kupungua. Uvivu wa kusoma
uliokuwepo tangia zamani unazidi kuiva na kuota nywele, vipele
na manyasi. Mmoja wa waandishi mashuhuri wa riwaya
nchini William Mkufya kasema katika jarida jipya la fasihi ,
SOMA, kuwa idadi ya Watanzania zaidi ya milioni 44 wanaosoma imepungua kwa asilimia 50
karibuni.
Mtazamo kwa wengi unamaanisha tunasoma tu tukiwa shule, kufaulu
mitihani. Tukishamaliza shule basi tena kitabu hakishikwi,
kinaonekana utoto; hakuna muda. Kazi inayojitokeza ni kunyoosha mikono miwili
kupokea pombe, kazi, kulea, kukaa barazani kupiga soga. Haya yote ni
muhimu ndiyo; lakini ukweli mmoja.
Kusoma ni sehemu mahsusi ya maendeleo ya jamii yeyote duniani. Na
kusoma si tu kwa ajili ya elimu-ufundi au elimu-taaluma bali kusoma
kujifunaisha kilugha na kistarehe. Haya hupatikana ndani
ya fasihi, tamthiliya, sinema, muziki na sanaa.
Moja ya matokeo ya tatizo hili kubwa la kutokusoma fasihi na hadithi za
kubuni linaonekana namna leo watu wengi (wazee kwa vijana; viongozi,
wanasiasa , waandishi wa habari na wataalamu) wasivyoweza kuandika au
kusema sentensi chache bila kuchanganya changanya maneno ya Kiswahili na
Kiingereza. Bado sisi wabovu tunadhani tutaeleweka zaidi ( na kuonekana
wajanja) tukiandika Kiswahili hapa; Kiingereza (kibovu) pale; Kiingereza hapa
na Kiswahili (kibovu) kule. Ulemavu huu unatokana na kukosa msamiati.
Tunapoendelea kupokea njia hizi za mawasiliano, lazima tuangalie ni kwa
namna gani hazitaathiri fikira zetu kulingana na utamaduni wetu. Si busara
kumnunulia mtoto ki-komputaa cha kuchezea ‘gemu’ badala yake tumnunulie kitabu.
Wakizoezwa hivyo tutakuwa tunajenga Taifa lenye watu wanaofikiri kama watu
wenye utu.
Watoto wakuuzwe njia za kuwafanya wawe watu wa kufiri na si u kupokea
madubwasha kutoka ng’ambo na kuyashabikia kana kwamba yanazalishwa Tanda Tundale.
Nafasi hiyo itawapa watot uwezo wa
kufikiri, kuunda kuvumbua, kuumba. Elimu ni mchakato endelevu wa
kuuondoa ujinga.
……………………………..Mwisho………………..
No comments