SIMBA,YANGA DIMBANI WEEKEND HII KOMBE LA SHIRIKISHO,RATIBA IKO HAPA
Mzunguko wa tatu wa michuano wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) unatarajiwa kuendelea
wikiendi hii mpaka katikati ya juma lijalo kwa michezo 13 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Kesho Jumamosi michezo mitatu itachezwa,
mjini Morogoro Burkinfaso FC watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa
Jamhuri mjini humo, Pamba FC watawakaribisha Toto Africans uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza, huku Ndanda FC wakichea dhidi ya Mshikamno FC
katika uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara.
Jumapili michuano hiyo itaendelea kwa
michezo mitatu, jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha
Friends Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji watakua wenyeji wa Tanzania
Prisons uwanja wa Amani Njombe, huku Stand United wakicheza dhidi ya
Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Michuano hiyo itaendelea Jumatatu,
Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora, Panone FC dhidi ya Madini FC uwanja wa Ushirika
mjini Moshi na Africa Lyon wakiwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Karume
jijini Dar es salaam.
Jumanne Mtibwa Sugar watawakaribisha
Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu
uwanja wa Wambi Mafinga, Africa Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani
jijini Tanga, na Geita Gold watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika
uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Singida United watacheza dhidi ya
Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa Namfua mjini Singida, na
mchezo wa mwisho utachezwa Februari 10 katika ya Wenda FC dhidi ya Mbeya
City uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mpaka sasa timu ya JKT Mlale pekee ndio
imeshafuzu kwa mzunguko wa nne baada ya kuiondosha Majimaji kwa mabao
2-1, katia mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Majimaji
mjini Songea.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KLABU YA PRISONS
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa klabu ya
Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kufuatia kifo cha
Mwenyekiti wake Hassan Mlilo kilichotokea jana katika hospital ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole
familia ya marehemu Hassan Mlilo, ndugu, jamaa, marafiki na klabu ya
Tanzania Prisons, na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu
nchini amesema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha
maombolezo.
Mwili wa marehemu Hassan Mlilo
unatarajiwa kusafirishwa leo mchana kuelekea mkoani Mbeya, ambapo
mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika mji wa Rujewa mkoani humo.
No comments