Amisi
Tambwe akikabidhiwa mpira ambao haukuwa miongoni mwa ile iliyotumika
kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya mschezaji huyo kufunga
magoli matatu kwenye mechi hiyo
Katika hali isiyo ya kawaida mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe jana
alipewa mpira feki na mwamuzi John Fannuel aliyechezesha mchezo wa jana
(January 21, 2016) kati ya Yanga dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa
taifa, Dar es Salaam.
Tambwe alifunga magoli matatu kwenye mchezo huo ambao Yanga walipata
ushindi wa mago 5-0 dhidi ya Majimaji. Kwa mujibu wa kanuni za soka,
mchezaji anayefunga magoli zaidi ya mawili hupewa mpira mmoja kati ya
ile ambayo ilitumika kwenye mchezo husika. Huu
ndiyo mpira aliopewa Tambwe kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya
kupiga hat-trick, mpira huu si miongoni mwa mipira inayochezewa kwenye
ligi msimu huu
Lakini jana mambo yalikuwa tofauti, wakati mwamuzi wa mchezo huo
anamkabidhi Tambwe mpira wake, mshambuliaji huyo alishtuka kwamba mpira
aliopewa haukuwa miongoni mwa ile iliyotumika kwenye mchezo wao dhidi ya
Majimaji. Alipodai mpira uliotumika kuchezea mchezo husika mwamuzi
alitia ngumu.
Baada ya kugundua ujanja huo uliofanywa na mwamuzi, mtandao huu
ulimfuata mwamuzi huyo na kumuuliza kwanini Tambwe hakukabidhiwa mpira
uliotumika kwenye mechi ya Yanga na Majimaji? Mwamuzi huyo alisema huo
ndiyo utaratibu uliopo na kama kuna maswali zaidi basi waulizwe
wasimamizi wa ligi. Amisi
Tambwe akikabidhiwa mpira na mwamuzi Ludovic Charles baada ya mchezaji
huyo kufunga magoli matatu kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand
United. Mpira huu ulkikuwa ni miongoni mwa mipira inayotumiwa kwenye
ligi ya msimu huu wa 2015-2016
Mbali na hayo, Tambwe alisema hat trick yake inamwendea moja kwa moja
mchumba wake. Hat-trick hiyo ni ya pili kwa Tambwe msimu huu, nyota
huyo alipiga bao tatu kwa mara kwanza kwenye msimu huu December 19, 2015
wakati Yanga ilipocheza na Stand United na ku-dedicate bao hizo tatu
kwa mtoto wake.
Kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand United Tambwe alikabidhiwa
mpira uliotumika kwenye mchezo huzika lakini cha kushangaza ni mpira
aliopewa jana ambao haukuwa miongoni mwa ile inayotumiwa kwenye ligi
msimu huu. Mshambuliaji
wa Yanga Amis Tambwe akionesha mpira kwa mashabiki baada ya kukabidhiwa
na mwamuzi. Huo ulikuwa ni mpira halisi tofauti na aliopewa kwenye
mchezo wa Yanga hidi ya Majimaj
TAMBWE APEWA MPIRA WA ‘KICHINA’
Reviewed by
Unknown
on
3:07 AM
Rating:
5
No comments