Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Idadi ya waliofariki Ghana yafikia 175

Takriban watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima. Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena. Ghana moto Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

No comments