Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Yanga yaendelea kupiga pesa

Yanga yaendelea kupiga pesa kupitia mauzo ya jezi ya wachezaji wake wapya iliyowasajili,toka iingie sokoni tarehe 25 may ,jezi ya Deus David Kaseke imeendelea kufanya vizuri kupitia jezi ya wakubwa (kiume) inayouzwa 30,000,ya kike inayouzwa 25,000 na watoto inauzwa 20,000 katika ripoti ya klabu imeripotiwa hadi sasa zimeuzwa jezi 6300 wastani wa takribani jezi 30 kila siku katika kila mkoa nchini Tanzania hivyo Mabingwa hao wa kihistoria Tanzania bara wameingiza fedha 157,500,000 Tshs kwa mauzo tu ya jezi ya mchezaji huyo aliyenunuliwa 35,000,000 Tshs. Wakati huo huo jezi ya Mshambuliaji mpya aliyejiunga na Yanga hapo jana 30 May hadi kufika usiku wa saa 5 jumla zilikuwa zimeuzwa jezi 120 katika mikoa yote Tanzania wastani wa jezi 4 kwa kila mkoa,zikipatikana katika maduka wakala wa vifaa vya michezo wa klabu hiyo,hadi sasa Mauzo ya jezi ya Busungu imeingiza pesa 3,000,000 Tshs ndani ya masaa 4. Nikiwa nami najiandaa kwenda kununua jezi iliyoandikwa BUSUNGU pale mitaa ya Mwanjelwa Mbeya lililopo duka wakala wa vifaa vya Yanga ,baada ya kununua ile ya KASEKE ili nikawatambie watani ambao mauzo ya jezi zao yamedorora kwa kuwa wanasajili wachezaji wa Mafungu Ghaflaaaaa nashtuka toka usingizini!zile hela nilizokuwa nazichekelea kuwa klabu imeingiza kupitia mauzo ya jezi ya KASEKE kumbe ni ndoto,yale mauzo ya jezi niliyodhani klabu itaingiza kupitia jezi ya BUSUNGU ikiwa tu siku ya kwanza imepatikana milioni 3 kumbe hakuna kitu kama hicho.Dah sasa klabu itaingiza kipato kupitia chanzo kipi kama hata hii njia ya mauzo ya jezi ambayo ni rahisi lakini wanashindwa?? Kwa sababu Teknolojia nchini kwetu ni ndogo lakini tungekuwa na mipango thabiti,nia ya kuipeleka Yanga mbele kama falsafa ya klabu yetu kuwa mbele daima basi tungefanya hivi,mara baada ya kumalizana na mchezaji husika inakuwa siri nzito miongoni mwa viongozi wetu waliokula yamini ya kuifanya Yanga iwe ya kimataifa kweli,mzigo wa jezi unachapishwa kimya kimya halafu unasambazwa katika maduka mbalimbali nchini nzima kama yanavyosambazwa magazeti !baada ya usambazaji kukamilika ndipo klabu yetu inatangaza usajili wa mchezaji husika kisha kuwaambia Jezi za mchezaji husika hupatikana maduka yote wakala wa vifaa vya michezo ya klabu yetu!hebu fikiria jumapili ya leo huko mikoani na jijini wangapi wangevaa jezi ya BUSUNGU ili kumnanga mtani wetu??wananchi tulivyo wengi na tunavyoipenda timu yetu nna uhakika zaidi ya piece 1200 zingeuzwa siku ya leo wastani wa piece 40 kila mkoa ingepatikana 30,000,000 Tshs jumla tungekuwa tusharudisha pesa tuliyomnunulia halafu tunakula faida. Wameahidi wengi lakini hawajatekeleza mpango huu,sidhani kama klabu ingeendelea kutegemea hela ya ufadhili kama tungethubutu kuwa na mipango hii.Acha nimalizie usingizi wangu uliokatishwa na ndoto nzuri ya mafanikio kuhusu klabu Yangu niipendayo. Yanga yaendelea kupiga pesa kupitia mauzo ya jezi ya wachezaji wake wapya iliyowasajili,toka iingie sokoni tarehe 25 may ,jezi ya Deus David Kaseke imeendelea kufanya vizuri kupitia jezi ya wakubwa (kiume) inayouzwa 30,000,ya kike inayouzwa 25,000 na watoto inauzwa 20,000 katika ripoti ya klabu imeripotiwa hadi sasa zimeuzwa jezi 6300 wastani wa takribani jezi 30 kila siku katika kila mkoa nchini Tanzania hivyo Mabingwa hao wa kihistoria Tanzania bara wameingiza fedha 157,500,000 Tshs kwa mauzo tu ya jezi ya mchezaji huyo aliyenunuliwa 35,000,000 Tshs. Wakati huo huo jezi ya Mshambuliaji mpya aliyejiunga na Yanga hapo jana 30 May hadi kufika usiku wa saa 5 jumla zilikuwa zimeuzwa jezi 120 katika mikoa yote Tanzania wastani wa jezi 4 kwa kila mkoa,zikipatikana katika maduka wakala wa vifaa vya michezo wa klabu hiyo,hadi sasa Mauzo ya jezi ya Busungu imeingiza pesa 3,000,000 Tshs ndani ya masaa 4. Nikiwa nami najiandaa kwenda kununua jezi iliyoandikwa BUSUNGU pale mitaa ya Mwanjelwa Mbeya lililopo duka wakala wa vifaa vya Yanga ,baada ya kununua ile ya KASEKE ili nikawatambie watani ambao mauzo ya jezi zao yamedorora kwa kuwa wanasajili wachezaji wa Mafungu Ghaflaaaaa nashtuka toka usingizini!zile hela nilizokuwa nazichekelea kuwa klabu imeingiza kupitia mauzo ya jezi ya KASEKE kumbe ni ndoto,yale mauzo ya jezi niliyodhani klabu itaingiza kupitia jezi ya BUSUNGU ikiwa tu siku ya kwanza imepatikana milioni 3 kumbe hakuna kitu kama hicho.Dah sasa klabu itaingiza kipato kupitia chanzo kipi kama hata hii njia ya mauzo ya jezi ambayo ni rahisi lakini wanashindwa?? Kwa sababu Teknolojia nchini kwetu ni ndogo lakini tungekuwa na mipango thabiti,nia ya kuipeleka Yanga mbele kama falsafa ya klabu yetu kuwa mbele daima basi tungefanya hivi,mara baada ya kumalizana na mchezaji husika inakuwa siri nzito miongoni mwa viongozi wetu waliokula yamini ya kuifanya Yanga iwe ya kimataifa kweli,mzigo wa jezi unachapishwa kimya kimya halafu unasambazwa katika maduka mbalimbali nchini nzima kama yanavyosambazwa magazeti !baada ya usambazaji kukamilika ndipo klabu yetu inatangaza usajili wa mchezaji husika kisha kuwaambia Jezi za mchezaji husika hupatikana maduka yote wakala wa vifaa vya michezo ya klabu yetu!hebu fikiria jumapili ya leo huko mikoani na jijini wangapi wangevaa jezi ya BUSUNGU ili kumnanga mtani wetu??wananchi tulivyo wengi na tunavyoipenda timu yetu nna uhakika zaidi ya piece 1200 zingeuzwa siku ya leo wastani wa piece 40 kila mkoa ingepatikana 30,000,000 Tshs jumla tungekuwa tusharudisha pesa tuliyomnunulia halafu tunakula faida. Wameahidi wengi lakini hawajatekeleza mpango huu,sidhani kama klabu ingeendelea kutegemea hela ya ufadhili kama tungethubutu kuwa na mipango hii.Acha nimalizie usingizi wangu uliokatishwa na ndoto nzuri ya mafanikio kuhusu klabu Yangu niipendayo.
Admin mlowezi swakala

No comments