Kuelekea mchezo wa Simba Vs Yanga Feb 20, hivi ni vibonzo 9 ambavyo hutumiwa na mashabiki kutaniana (+Pichaz)
Mtu wangu wa nguvu kwa wapenzi wa soka la Bongo kwa sasa ni kuhusu mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumamosi ya February 20 katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, mchezo ambao unazikutanisha timu zote zenye nafasi ya kutwa Ubimgwa wa Ligi Kuu, huu ni mchezo wa marudiano na kisasi kwa Simba, au Yanga waendeleze ubabe baada ya mchezo wa awali Simba kukubali kufungwa kwa jumla ya goli 2-0.
Kwa sasa Simba wapo nafasi ya kwanza wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na jumla ya point 45 katika mechi zao 19 walizocheza, lakini Yanga
wapo nafasi ya pili wakiwa na point 43 katika michezo yao 18 waliocheza
wakiwa na kiporo cha mchezo mmoja. Huo ni mchezo wenye utani, presha
kwa mashabiki na kejeli za hapa na pale. Mtu wangu wa nguvu tukiwa
tunaelekea mchezo huo, enjoy kwa vibonzo 9 ambavyohutumiwa na mashabiki
wa Simba na Yanga kutania mitandaoni baada ya mchezo kumalizika na mmoja kati ya timu hizo akiwa kaibuka mshindi.
No comments