Leo nchini Tanzania Rais wa nchi hiyo Jakaya
Kikwete atawaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa
Bunge la jamhuri ya muungano Tanzania Captain John Komba aliyefariki
ghafla jumamosi jijini Dar es salaam.
Mwili wa Marehemu utasafirishwa kwenda Wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma kusini mwa Tanzania.
Mbali ya kuwa mwanasiasa alikuwa pia msanii maarufu mwimbaji akioongoza kikundi cha muziki cha Tanzania One Theater.
Mwandishi
wetu Arnold Kayanda amefika nyumbani kwa marehemu katika eneo la Mbezi
Beach jijini Dar es Salaam na hii ni taarifa yake.
No comments