Alichoongea Jerry Murro mchana wa leo.
"Tumefuatilia hatua zote kwa umakini utaratibu uliotumika kumchezesha
Ibrahimu Ajibu tumegundua ni kumefanyika figisu figisu juu ya swala
hili, hakuna utaratibu uliopitishwa wa mchezaji kuchagua mechi za
kutumikia adhabu yake , sio katibu wala rais wa TFF anayeijua na
kuiidhinisha hii sheria hadi hao Simba waitumie,tumetafuta ofisi ya rais
kama kutakuwepo na nyaraka hiyo hakuna, wala wajumbe wa bodi hawajui
tulichogundua ni watu wachache
wakakutana na kupindisha sheria hii,kama wataleta nyaraka iliyoruhusu
sheria hii kutumika tena ikiwa imesainiwa na rais wa TFF mimi ntaachia
ngazi ntajiuzulu wadhifa wangu katika klabu ya Yanga,kwa kuwa sisi hii
ligi pia inatuhusu tunaiagiza TFF mara moja kuipoka pointi Simba na
kuwapa Prison,kiongozi wa Simba aliyedanganya kwa kuandika barua naye
aadhibiwe kwani amehusika kumhadaa Fatma Ramadhani na pia kumpotosha
Mchezaji Ibrahimu Ajibu akacheza katika mechi yake ambayo ni batili
kwake pia rais Jamal Malinzi aivunje kamati hii. . "
Mkuu huyo wa kitengo cha habari cha klabu Yanga aliendelea kwa kusema
"Kwa kawaida ratiba ibadilishwapo huitwa vilabu husika hukaa pamoja na bodi ya ligi huchagua tarehe nyingine ya mchezo huo, lakini bodi hii haijafanya hivo wala hakuna e mail waliyovitumia vilabu hivi kuvitaarifu zaidi tunasikia kwenye mitandao ya kijamii,hata kaimu afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Fatma Abdallah alipouliza kama kaufuata utaratibu huu haelewi, kwa kweli huyu mama mambo mengi sana yanamshinda kiatu alichovaa sio saizi yake tunaomba achie ngazi wasimamie watu wanaojua amekuwa kiini cha uharibifu wa ligi yetu, tulipokuwa Nairobi kutokea Botswana tulisikia hata mechi yetu dhidi ya Simba itasogezwa mbele ndipo tukamuuliza Ayoub Nyenzi mjumbe wa TFF naye akawasiliana na viongozi wa TFF ambao walimjibu kuwa hakuna mabadiliko yoyote kwa mechi za Yanga lakini ajabu na kweli kesho yake tunasikia mechi imeahirishwa, tunasema hatuwezi kufumbia macho uvunjifu huu wa sheria na hatutoleta timu uwanjani march 11"alimalizia Jerry Murro

No comments