PICHA: Sugu kazindua Ligi ya Professor Jay, Buffalo FC ikiiadhibu Magomeni
Ligi ya mbunge wa Mikumi Morogoro Joseph Haule ambaye wengi tunamfahamu kwa jina lake la muziki Professor Jay imezindulia Jumapili ya November 27 2016 na waziri kivuli wa habari na michezo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Uzinduzi huo ambapo Professor Jay na Sugu walishirkiana kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, ulizinduliwa kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya Buffalo FC kutoka kijiji cha Doma dhidi ya timu ya Magomeni Stars kutoka kata ya Magomeni, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Buffalo FC kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
No comments