Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Yanga yaikalisha MO Bejaia

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Afrika ngazi ya klabu, Yanga wameweka hai matumaini kiduchu ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali baada ya kuibwaga MO Bejaia.
image
Shujaa wa Yanga katika mchezo wa leo alikuwa n mshambuliaji Amissi Tambwe aliyefunga bao pekee na kuipa timu yake ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Simon Msuva aliunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Abdul na kuwababatiza walinzi wa MO Bejaia na Tambwe kuumalizia nyavuni.
Kwa ushindi wa leo, Yanga imefikisha pointi nne na kuendelea kuvuta mkia licha ya kuweka hai matumaini kiduchu ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali kutegemeana na matokeo ya TP Mazembe.

No comments