Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

NDONDO CUP 16 BORA NI MKWANJA KWENDA MBELE

IMG-20160629-WA0020
Utepe wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup umekatwa leo kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii zamani ukijulikana kama Bandari au wenye wenye huuita Wembley pale maeneo ya Tandika. Mchezo wa ufunguzi wa hatua hiyo ulizikutanisha Faru Jeuri dhidi ya Temeke Squad na dakika 90 kumalizika kwa mabingwa watetezi Faru Jeuri kupata nafasi ya kutinga katika hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0.
Faru Jeuri ndiyo walikuwa wakwanza kujipatia magoli yao kipindi cha kwanza kupitia kwa Masamaki Juma lakini baadaye kipindi cha pili Jerome Lambele akafanikiwa kuifungia timu yake magoli mawili.
IMG-20160629-WA0017
Dakika zikiwa zinayoyoma, Temeke Squad wakajipatia bao la kufutia machozi lililofungwa kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Twalib Kabuluma na mchezo ukamalizika kwa Faru Jeuri kuibuka na ushindi.
Katika hatua hii mambo mengi yamejiri kwenye uwanja wa Bandari ambapo mashabiki waliokuwa wanaingia kwenye uwanjani kwa kiingilio chao cha shilingi 2000 walikuwa wanapata nakala ya gazeti maalum la Mwanaspoti ambalo lenyewe litolewa likiwa limesheheni matukio mbalimbali ya michuano ya Ndondo Cup.
IMG-20160629-WA0015
Kuanzia hatua ya 16 bora, anatafutwa mchezaji bora wa kila mechi zoezi ambalo limeanza leo ambapo Jerome Lambele ameibuka mchezaji bora wa mechi ya leo na kupata kitita cha shilingi 50,000 taslim kutoka kwa Mwanaspoti lakini zawadi hiyo ikiambatana na kofia pamoja na T-shirt kutoka kwa wadhamini.
Lakini mambo ya ‘mtonyo’ hayakuishia hapo, Startimes nao pia wameingia kwenye mashindano hayo na wanamwaga mpunga. Timu ambayo imefanikiwa kushida imeondoka na kitita cha shilingi 300,000 wakati waliofungwa wamechukuwa shililingi 200,000.
IMG-20160629-WA0014
Kunazia hatua hii ya Sports Extra Ndondo Cup hakuna timu ambayo itaondoka bila mshiko, mtonyo nje-nje kuanzia kwa timu hadi wachezaji.
Mchezaji bora wa mechi hii Jerome Lambele alizungumza machache baada ya kuibunga nyota wa mchezo: “Inatoa changamoto, haya ni mashindano unapopata nafasi kama hii ya kuwa mchezaji bora ni jambo la kujivunia. Nimeshawahi kuwa mchezaji bora wa mechi katika mashindano tofautitofauti.”
IMG-20160629-WA0016
“Sisi bado tunapambana na kuanzia hatua hii ukipigwa unatoka, kwahiyo tunaendelea kujipanga kutetea ubingwa wetu.”

No comments