Wachezaji wa Leicester walivyowasili nyumbani kwa Vardy na kuanza kusherehekea Ubingwa
Baada ya klabu ya Leicester City kutangaza Ubingwa kufuatia sare ya goli 2-2 waliotoka Tottenham Hotspurs dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge, wachezaji wa Leicester City kwa pamoja walikusanyika katika nyumba ya Jamie Vardy ambaye ni mchezaji mwenzao wa timu hiyo na kuanza kusherekea.
Nyota karibia wote wa Leicester City waliwasili kwa Vardy huku baadhi ya mashabiki wakiishia kuzunguuka nyumba ya Vardy na kushangazwa na wachezaji hao wa Leicester City ambao wametwaa Ubingwa mbele ya timu vigogo kama Chelsea, Man United Arsenal na nyinginezo.
No comments