Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Wanaume wawili wafiwa na Mke wao





Mkazi wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda kupatiwa matibabu kwa kaka yake.
Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.
Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.
“Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.
Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.
Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

No comments