Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

TAARIFA KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2015 ,SOMA HAPA



Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwakwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016

.
Baraza la Mitihani la Tanzanialinapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.

Hivyo,Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo.


Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato Utakapokamilika



Imetolewa na,

AFISA HABARI NA UHUSIANO

No comments