Mbwana Samatta acheza mechi yake ya kwanza akiwa na KRC Genk ya Ubelgiji, huu ndio ushindi walioupata (+Pichaz)

Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena leo
February 6 kwa michezo kadhaa kupigwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa
leo February 6 ni mchezo kati ya Mouscron FC dhidi ya klabu ya KRC Genk
inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo huu ulikuwa na mvuto
kwa Tanzania zaidi kwani ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta kucheza
toka amejiunga na klabu hiyo.

Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mpya
wa timu ya taifa ya Tanzania, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na
klabu yake mpya ya KRC Genk akitokea benchi, Samatta aliingia dakika ya
73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis ambaye alitoa pasi ya goli la
ushindi kwa KRC Genk dakika ya 63 na Thomas Buffel kupachika mpira
nyavuni.

Mchezo ulimalizika kwa KRC Genk
kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mouscron, lakini
hadi mpira unamalizika Mouscron walikuwa wanaoongoza kwa kumiliki mpira
kwa asilimia 53 na KRC Genk asilimia 47, ushindi huo umeifanya Genk
kutimiza jumla ya point 38 na kusogea hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa
Ligi.





No comments