Kama ulikuwa unajua soka la wanawake limetupwa, TFF wamefikia hapa Feb 23 2016

Shirikisho la soka Tanzania TFF February
23 limefanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuingia
mkataba na Karibu Tanzania Association kwa ajili ya maendeleo ya soka la
wanawake ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kuwa nyuma kwa upande wa
Tanzania.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Mia walipokuwa wakiongea mbele ya waandishi wa habari
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Rais
wa TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wameingia
makubaliano na katibu wa TFF Selestine Mwesigwa kusaini mkataba na
kusaini mkataba na Mia Mjengwa ambae ni mshauri wa Karibu Tanzania
Association.

Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisaini mkataba
Mkataba huo ni endelevu na mafunzo ya
soka yataanza kutolewa kwa shule za kijamii. Baada ya kumalizika kwa
mkutano huo Rais wa TFF Jamal Malinzi aliomba watu kuwa watulivu na
kusubiri hadi March 30 ndio kesi ya tuhuma za upangaji wa matokeo kwa
michezo ya mwisho ya mechi za Ligi daraja la kwanza itasikilizwa.

Mshauri wa KTA Mia Mjengwa akisaini mkataba
No comments