Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Jaji wa korti ya juu Kenya asimamishwa kazi


Image caption Jaji Philip Tunoi
Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi jaji wa mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi.
Rais Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji Phillip Tunoi na akateua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.
Jaji adaiwa kupokea rushwa ya $2m KenyaJopo la kumchunguza jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu.
Jaji
Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir, Jaji Mstaafu Jonathan Havelock, Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.
Jaji Tunoi amekanusha madai dhidi yake.

No comments