Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Yanga waendeleza ubabe wao dhidi ya Mbeya City, cheki pichaz na matokeo ya mechi za Ligi Kuu TZ Dec 26

Ligi Kuu soka Tanzania imeendelea uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Dar Es Salaam Young Africans kuwakaribisha wagonga nyundo wa jiji la Mbeya klabu ya Mbeya City. Huu ni mchezo wa 13 kwa klabu ya Yanga ambao ndio wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi.
DSC_0032
Juma Kaseja akielekea kuudaka mpira miguu kwa beki wake ili Amissi Tambwe asije kuleta madhara.
Yanga ambao ndio wanatajwa kuwa na kikosi bora msimu huu wa Ligi waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga klabu ya Stand United kwa jumla ya goli 4-0. December 26 Yanga wameendeleza rekodi yao ya ushindi baada ya kuiadhibu Mbeya City iliyokuwa nafasi ya 10 huku ikiwa na point 11 kwa jumla ya goli 3-0.
DSC_0033
Donald Ngoma akichuana na Tumba Sued alioneshwa kadi nyekundu kipindi cha pili kwa kosa la kumfanyia faulo ya makusudi Ngoma.
Licha ya kuwa klabu ya Mbeya City ilianza kwa kucheza mchezo wa kujihami zaidi kabla ya dakika ya 36 kwenda mbela kushambulia na Simon Msuva wa Yanga akaupata mpira na kutoa pasi nzuri kwa Amissi Tambwe na kupata goli la uongozi, kipindi cha mabo yalizidi kwenda mlama kwa upande wa Mbeya City baada ya Amissi Tambwe kupachika goli la pili na dakika moja baadae Thabani Kamusoko akaitimisha kwa kufunga goli la tatu.
DSC_0037
Simon Msuva akitafuta namna ya kumtoka beki wa Mbeya City
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa December 26
  • Mwadui FC 1-1 Simba
  • Ndanda FC 1 – 3 JKT Ruvu
  • Coastal Union 1 – 3 Stand United
  • Maji Maji FC 0 – 2 Prisons
  • Mtibwa Sugar 3 – 0 Mgambo JKT
DSC_0053
Deus Kaseke wa Yanga akidhibitiwa vilivyo na beki wa Mbeya City

No comments