Sema Ghana wametisha sana na hii kampuni inayotengeneza magari.. ( picha 14 )

Kampuni inaitwa Kantanka Group na mpaka sasa wanaweza kutengeneza magari mapya mia moja kila mwezi… pia gari la bei rahisi zaidi linagharimu MILIONI 40 za Kitanzania.

Mafundi wakiwa kwenye moja ya hatua za kuunda gari

Zamani watoto wa kiafrika walikua wakionekana kuunda magari yao ya mbao lakini ukiyatazama unaona kabisa akili iliyotumika hapa sio ya kawaida, wengine walijaribu hata kuunda ndege na Helikopta Kenya na Nigeria ila sasa ndoto zimeanza kutimizwa….. naamini hii itawapa wengine nguvu ya kujiamini na kujaribu.



Hii ni moja ya aina ya magari yaliyotengenezwa na kampuni hii ya Ghana.






Magari yenyewe wanayoyatengeneza


Picha zote ni kutoka CNN.
No comments