Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

Ripoti kutoka Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam kwenye Kesi ya Mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona..

July 06 2015 ilisambazwa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuhusu Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam kutoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja kwa Mawaziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba, na Daniel Yona baada ya kukutwa na hatia ya Kesi ya  kuisababishia hasara Serikali pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Screen-Shot-2015-07-06-at-4.23.50-PM
Basil Mramba, Daniel Yona na Grey Mgonja wakiwa nje ya mahakama ya Kisutu kusubiri kuingia ndani kabla ya Kesi yao kusikilizwa July 6 2015.
Mbali na hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, Mramba na Yona walitakiwa pia kulipa faini ya Milioni tano kila mmoja.
Ninayo Ripoti nyingine kutoka Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam… Rufaa ya Kesi hiyo imefikishwa kwenye meza ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama hiyo imeikataa Rufaa hiyo.
Kingine kilichoamriwa ni kwamba watuhumiwa wote wawili wamepunguziwa adhabu ya kifungo, kwa sasa watatumikia miaka miwili jela na adhabu ya faini imeondolewa.
Screen-Shot-2015-07-06-at-4.25.23-PM
Screen-Shot-2015-07-06-at-4.25.14-PM
Source: Millard Ayo

No comments