Pale ambapo Refa anaamua kutumia Bastola baada ya mambo kuharibika Uwanjani..

Mara nyingi tumezoea kuona waamuzi
wakitumia madaraka yao kuwaonya wachezaji soka uwanjani kwa kadi za
manjano na kadi nyekundu kama kosa ni kubwa, lakini hii imekuwa tofauti
kidogo kwa muamuzi Gabriel Murta ambaye alitumia zaidi ya kadi na filimbi kujihami uwanjani.
Gabriel Murta
alipatwa na hasira uwanjani na inadaiwa alienda katika vyumba vya
kubadilishia nguo na kurudi na bastola uwanjani huku akimuonyeshea moja
kati ya wachezaji waliokuwa wakicheza mechi hiyo, tukio hilo lilitokea
katika Ligi za madaraja ya chini Brazil, kwani ilikuwa ni mechi kati ya Brumadinho dhidi ya Amantes da Bola.
Video ya tukio hilo ilirekodiwa na moja
kati ya mashabiki waliokuwa wamehudhuria mchezo huo, stori kutoka kwa
watu waliokuwemo katika mchezo huo ni kuwa, tukio hilo lilitokea baada
ya viongozi wa klabu ya Amantes da Bola kuvamia uwanja na kumshinikiza Murta kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa timu pinzani.
Meneja wa chama cha waamuzi Giuliano Bozzano
amenukuliwa akisema kuwa muamuzi huyo alitoa bastola uwanjani ili
kujihami mwenyewe, kwani kulikuwa na uwezekano wa kufanyiwa vurugu na
wachezaji na viongozi wa klabu ya Amantes da Bola waliokuwa wameingia uwanjani. kufuatia tukio hilo Gabriel Murta ambaye alikuwa muamuzi wa mechi hiyo, huenda akafungiwa kujihusisha na soka kwa muda mrefu au maishaSource: Millard Ayo
No comments