Mama wa mapacha watatu katelekeza watoto wote Hospital, anahofia malezi? Aliporudi kayajibu haya..

Kwa Tanzania ni kosa la jinai kutupa au
kutekeleza mtoto mchanga, na sio Tanzania pekeake, sehemu nyingi Duniani
ukitelekeza au kutupa mtoto sio kesi ya kusamehewa hata kidogo !!
Jeaneta Bente ni mama wa watoto mapacha watatu, alijifungua na kuwatelekeza watoto wake wote Hospitali iliyoko Jiji la Drobeta Turnu-Severin, nchi ya Romania.
Mama huyo alijifungua mapacha hao Alexandra, Isabela na Cristina
salama kabisa japo watoto wote walizaliwa njiti yani hawakutimia miezi
tisa… aliamua kutoroka na kukimbia Hospitali huku akiwatelekeza watoto
hao wachanga.

Baadae taarifa ya watoto kutelekezwa
ikagusa kwenye stori za Vyombo vya Habari, mama akaamua kurudi na
kuongea ukweli sababu iliyofanya awatelekeze watoto wake Hospitali
>>>’Naamini watu watanielewa
kwamba sina uwezo wa kuwatunza na kuwahudumia… Nawatakia kila la heri na
ninaamini watakuwa na maisha mazuri zaidi ya vile ambayo mimi
ningewalea‘ >>> hii ndio sentensi aliyonukuliwa Jeaneta Bente akijitetea kuhusu kuwatelekeza watoto wake.

Ripoti za Hospitali za Romania
zinaonesha kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaotelekezwa na wazazi
wao huku wakitoa sababu moja kubwa kwamba hawna uwezo wa kuwalea watoto
wao.
Hizi ni pichaz za mazingira ya mama huyo anapoishi.


No comments