Muingereza aliyepona Ebola kurejea Afrika
Mwanaume wa kwanza muingereza kuambukizwa homa kali ya Ebola, katika mlipuko wa ugonjwa huo unaoshuhudiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, anatarajiwa kurejea Afrika ambako aliambukizwa.
Anasema anafanya hivyo ili aweze kuwasaidia wengine walioathirika kuweza kupambana na ugonjwa huo ambao ni janga kubwa
William Pooley alipokea matibabu mjini London baada ya kupelekwa nchini humo kutoka Sierra Leone.
Ameweza kupona na hata kuodnoka hospitalini. Lakini kwa sasa anajiandaa kusafiri kurejea Afrika katika wiki chache zijazo.
Watu wamekuwa wakihamasishwa kujizuia na maambukizi kwa kuweka usafi
Pooley mwenye umri wa miaka 29, alisema ana hamu kubwa sana kurejea Afrika na kwamba huenda asiweze kuambikizwa.
Wakati Pooley alipoambukizwa, alikuwa anafanya kazi ya kujitolea nchini Sierra Leone, ambayo ni moja ya nchi za kanda ya Afrika Magharibi zilizoathriwa na ugonjwa huo.
Takribna nusu ya watu 3,000 waliombaukizwa homa hiyo, katika mlipuko wa sasa barani Afrika, ambao ilianzia nchini Guinea, wamefariki.
chanzo cha habari:BBC
Pololey amesema ana hamu sana kurejea Afrika kuwasaidia wagonjwa wengine
No comments