Kocha Maximo awajibu Simba.
KOCHA hodari kwenye kufanya uamuzi mgumu na mwenye misimamo ya aina yake, Mbrazili Marcio Maximo amejibu maswali ambayo wadau wengi walikuwa wakijiuliza juu ya mpango wake wa kuchezesha vikosi viwili katika mechi moja.
Katika mechi zake, Maximo amekuwa akichezesha timu mbili katika mechi moja ambayo moja huanza dakika 45 za mwanzo na nyingine hucheza dakika 45 za mwisho.
Wadau walikuwa wakihoji juu ya staili yake hiyo ambayo ilikuwa inashuhudiwa na wapinzani wake wakuu Simba pamoja na mashushushu wa klabu nyingine za Ligi Kuu Bara.
Bosi huyo anasema moja ya sababu ni kuwaweka wachezaji wote katika hali ya kuwa fiti kwani yapo matatizo mengi hujitokeza mfano ni majeruhi na wakati mwingine wachezaji kuitwa timu za taifa pia alitaka kufahamu vizuri kiwango cha kila mchezaji.
Akizungumza na Mwanaspoti, Maximo alisema: “Moja ya faida juu ya kuchezesha vikosi viwili ni kuwa na wachezaji walio tayari muda wote mfano wameitwa baadhi ya wachezaji kwenye timu ya Taifa kama nisipofanya hivi, wachezaji gani watacheza.”
“Lakini sasa sina wasiwasi hata kama hao watakwenda wapo wengine wataziba mapengo yao, ndiyo sababu kubwa lakini baada ya mechi hizi za Zanzibar, nitakuwa nikiwachezesha dakika 90,” alisema Maximo ambaye enzi zake akiikochi Taifa Stars aliwahi kuwapiga chini mastaa kama Juma Kaseja, Athuman Idd, Haruna Moshi ‘Boban’ ambao walikuwa kwenye fomu.
No comments