Tupashane Habari 24-hours

Tupashane Habari 24-hours

Breaking News

kampa kampa tena

ARSENE WENGER AZUNGUMZIA USHINDI,KADI NYEKUNDU NA OLIVIER GIROUD AMBAYE ATAKUWA NJE MPAKA MWAKA MPYA .

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa alijisikia nafuu baada ya ushindi wa jumla ya bao 1 -0 dhidi ya timu
ya Uturuki Beşiktaş katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi .

Pamoja na hayo pia wenger amethibitisha kuwa Olivier Giroud atakuwa nje mpaka mwaka mpya baada ya mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji juu ya kifundo cha mguu wake,kutokana kujeruhiwa katika mchezo wa jumamosi waliotoka sare ya  2-2 dhidi Everton,ambapo mchezaji huyo alipachika bao la kusawazisha.

Mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez alifunga bao muhimu ambalo liliwawezesha Arsenal kuendelea katika hatua ya makundi na  kufuzu kwa Mara ya Kumi na saba (17) Mfululizo katika michuano ya Klabu Bingwa ulaya.

"hatukuamini  mpaka ilipotokea na kisha kila mtu akajiuliza kwa nini alifanya hivyo kutokea ," 

"tuna wakati mzito ambao tumeubeba sasa kwa sababu sisi tumejikita sana katika Premier League, Tunasubiri droo kuchezeshwa'.
"Tulicheza dhidi ya timu nzuri na ilionyesha  mapambano".
"Tunahisi tumefanya kazi na tunadhamiri njema."Wenger aliiambia Sky Sports.
Arsenal alimaliza mechi na watu 10 baada ya Mathieu Debuchy akutolewa kwa kadi ya pili ya  njano - uamuzi ambao Wenger  amesema si mzuri kabisa .
"Nilikuwa na hofu sana kwa sababu huwezi kujua kama tuna baadhi ya wachezaji ambao wako vizuri kimwili," Wenger aliongeza.
"Mimi nadhani ilikuwa mbaya sana kwa sababu Debuchy alicheza mpira na labda (mwamuzi) alikuwa na  hasira dhidi yetu, kwenye benchi tuliona Debuchy alicheza mpira.
"Mwamuzi alikuwa kwa upande mwingine." Wenger alifafanua.
KUTOKA KWA Herman Kihwili.FACEBOOKMLOWEZI SWAKALA

No comments