KOMBE LA DUNIA: GERMANY, NIGERIA ZATANGAZA VIKOSI VYA AWALI!
GERMANY: MERTESACKER, PODOLSKI, OZIL WA ARSENAL NDANI, MARIO GOMEZ NJE!
NIGERIA: YOBO, ODEMWINGIE WAREJESHWA KUNDINI!
BAADA WENYEJI wa Fainali za Kombe la
Dunia zitakazochezwa kuanzia Juni 12, Brazil, kutangaza Kikosi chao cha
awali, Nchi za Germany na Nigeria nao wametangaza Vikosi vyao vya awali
vya Wachezaji 30 kila mmoja.
GERMANY
Wachezaji watatu wa Arsenal, Per
Mertesacker, Lukas Podolski na Mesut Ozil, ni miongoni mwa Wachezaji 30
waliotangazwa na Kocha, Joachim Low, kwenye Kikosi cha awali cha Germany
kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Mchezaji mwingine pekee toka Ligi Kuu England ni Andre Schurrle wa Chelsea.
Nae Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira
ametajwa licha ya kutocheza tangu Novemba alipoumia vibaya Goti lakini
Straika wa Fiorentina, Mario Gomez, ambae nae aliumia na kuwa nje kwa
Miezi 7 na tangu arejee Mwezi Septemba amekuwa akicheza kwa nadra,
hayumo kwenye Kikosi hicho.
Kwenye Kikosi hicho, Bayern Munich imetoa Wachezaji 7 na Dortmund Dortmund 6.
Kila Nchi inayocheza Fainali inatakiwa
ipeleke Majina ya Wachezaji wao wasiozidi 30 kwa FIFA ifikapo Mei 13 na
Listi ya mwisho ya Wachezaji 23 inatakiwa iwasilishwe Juni 2.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Neuer (Bayern Munich), Weidenfeller (Dortmund), Zieler (Hanover)
MABEKI: Boateng (Bayern
Munich), Durm (Dortmund), Grosskreutz (Dortmund), Hoewedes (Schalke),
Hummels (Dortmund), Jansen (Hamburg), Lahm (Bayern Munich), Mertesacker
(Arsenal), Mustafi (Sampdoria), Schmelzer (Dortmund).
VIUNGO: Bender
(Leverkusen), Draxler (Schalke), Ginter (Friburg), Goretzka (Schalke),
Goetze (Bayern Munich), Hahn (Augsburg), Khedira (Real Madrid), Kroos
(Bayern Munich), Meyer (Schalke), Muller (Bayern Munich), Ozil
(Arsenal), Podolski (Arsenal), Reus (Dortmund), Schurrle (Chelsea),
Schweinsteiger (Bayern Munich)
MAFOWADI: Klose (Lazio), Volland (Hoffenheim)
NIGERIA
Nigeria imewarejesha tena Kikosini
Joseph Yobo na Peter Odemwingie katika Kikosi chao cha awali cha
Wachezaji 30 cha Fainali za Kombe la Dunia.
Mara ya mwisho kwa Yobo kuichezea
Nigeria ni Mwaka Jana kwenye Fainali za AFCON huko Afrika Kusini wakati
Odemwingie, anaechezea Stoke City, amekuwa akiachwa na Kocha Stephen
Keshi baada kugomba nae tangu kabla ya AFCON 2013.
Wachezaji maarufu ambao wameachwa ni pamoja na Brown Ideye na Fegor Ogude wanaocheza Klabu za Ukraine.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Vincent Enyeama
(Lille/France), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva/Israel), Chigozie
Agbim (Gombe United, Nigeria), Daniel Akpeyi (Warri Wolves, Nigeria)
MABEKI: Elderson
Echiejile (Monaco/France), Efe Ambrose (Celtic FC/Scotland), Godfrey
Oboabona (Rizespor/Turkey), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves, Nigeria),
Kenneth Omeruo (Middlesbrough/England), Juwon Oshaniwa (Ashdod
FC/Israel), Joseph Yobo (Norwich City/England), Kunle Odunlami (Sunshine
Stars, Nigeria)
VIUNGO: Mikel Obi
(Chelsea/England), Ogenyi Onazi (SS Lazio/Italy), Ramon Azeez
(Almeria/Spain), Ejike Uzoenyi (Enugu Rangers, Nigeria), Gabriel Reuben
(Beveren/Belgium), Nosa Igiebor (Real Betis/Spain), Joel Obi
(Parma/Italy), Michael Uchebo (Cercle Brugge/Belgium), Sunday Mba (CA
Bastia/France)
MAFOWADI: Ahmed Musa
(CSKA Moscow/Russia), Shola Ameobi (Newcastle United/England), Victor
Moses (Liverpool/England), Emmanuel Emenike (Fenerbahce/Turkey), Obinna
Nsofor (Chievo Verona/Italy), Peter Osaze Odemwingie (Stoke
City/England), Babatunde Michael (Volyn/Ukraine), Nnamdi Oduamadi
(Varese/Italy), Uche Nwofor (Heerenveen/Netherlands)
No comments