Wanaume wawili wafiwa na Mke wao
Mkazi
wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica
Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki
dunia.Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki
iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda kupatiwa matibabu kwa kaka
yake.
Maganga
alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali
kuishi na mume mdogo.Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote
wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri
kuu katika nyumba yao.
Aliwataja
wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na
Arcado Mlele (47).Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika
kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani
mwa Chunya na Tabora.
“Baada
ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo
na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema
Maganga.Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati
yao wawili wa kike.
Maganga
alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa,
anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto
wengine watatu ni wa mume mkubwa.Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na
wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu
walizoeleka kwa wanakijiji.Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye
nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa
mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.“Mambo
ya kula, kunywa na mengine, mama alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo
mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao
walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.
Alisema
siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na
kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.Wakati wa
mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha
maswali mengi kwa jamii.
No comments