Mtu wangu wa nguvu najua umesikia au
unaelewa jinsi gari za viongozi wa juu wa serikali hususani marais
zinavyokuwa na thamani kubwa kutokana na hadhi na uhitaji wa gari zenye
usalama kwao. Basi mtu wangu wa nguvu katika pitapita zangu mtandaoni
nikakutana na
TOP 20 ya Ikulu 20 zinazotumia magari ya kifahari duniani. Huenda ukawa hujui Afrika kuna nchi mbili tu
Kenya na
Morocco ndio Ikulu zake zimeingia katika list ya magari 20 ya thamani zaidi duniani. Hii ni list kwa mujibu wa
therichest.com
20 – Kenya
Ikulu
ya Kenya wanatajwa kutumia Mercedes-Benz Pullman S600 bei yake inatajwa
kufikia dola 50,000 ambazo ni zaidi ya milioni 100 za Kitanzania
19 – Italia
Italia
wao wanatajwa kutumia gari aina ya Lancia Thesis yenye thamani ya dola
65,709 ambazo ni zaidi ya milioni 140 za kitanzania.
18 – Japan
Hii
ndio gari inayotumiwa na Ikulu ya Japan Toyota Century Royal thamani
yake ni dola 85,500 zaidi ya Tsh milioni 180 za kitanzania
17 – Singapore
Serikali
ya Singapore inatajwa kutumia gari aina ya Mercedes-Benz S350L yenye
thamani ya dola 85,995 ambazo ni zaidi ya milioni 185 za kitanzania.
16 – Uzbekistan
Ikulu ya Uzbekistan wanatumia Range Rover Supercharged bei yake ni dola 103,195 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 225
15 – Morocco
Kwa Morocco inatumiwa Mercedes 600 Pullman bei yake ni dola 120,384 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 260
14 – Korea Kusini
Korea
Kusini Hyundai Equus VL500 (550) Limousine yenye thamani ya dola
122,180 ndio inatumika katika nchi hiyo. yake thamani yake ni zaidi ya
Tsh milioni 265
13 – Norway
Norway wanatumia Binz Limousine yenye thamani ya dola 128,351 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 280
12 – Brunei
Hii inaitwa Rolls Royce Phantom VI ina thamani ya dola 148,645 ambazo ni zaidi Tsh milioni 320
11 – Ujerumani
Ikulu ya Ujerumani wanatumia Mercedes-Benz S600L thamani yake dola 174,890 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 380
10 – India
Mercedes-Benz S600 (W221) Pullman Guard thamani yake ni dola 180,000 zaidi ya Tsh milioni 390
9 – Philippines
Mercedes-Benz W221thamani yake dola 250,547 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 540
8 – Urusi
Mercedes S-Class Limousine thamani yake ni dola 251,417 zaidi ya Tsh milioni 545
7 – Malaysia
Maybach 62 thamani yake ni dola 394,000 zaidi ya Tsh milioni 850
6 – UK
Jaguar XJ Sentinel thamani yake dola 455,025 zaidi ya Tsh milioni 990
5 – Thailand
Maybach 62 Limousine thamani yake inafikia dola 500,000 zaidi ya Tsh bilioni 1
4 – Vatican
Mercedes-Benz M-Class bei yake inafikia dola 524,990 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.1
3 – China
China wanatumia Hongqi Limousine ya dola 801,624 zaidi ya Tsh bilioni 1.7
2 – USA
Cadillac One hii inatajwa kuuzwa dola milioni 1.5 na hutumiwa na Rais wa Marekani Barack Obama zaidi ya Tsh bilioni 3.2
1 – Malkia wa Uingereza ndio anatumia gari yenye thamani kuliko zote.
Bentley State Limousine inatumiwa na Malkia wa Uingereza thamani yake ni dola 15,167,500 zaidi ya Tsh bilioni 33
No comments