Chelsea inakaribia kumsajili staa huyu, wakati ambao Pedro anaanza safari ya kurudi Barcelona …
Stori kutoka katika mitandao mbalimbali
barani Ulaya hususani Uingereza, imekuwa ikiripoti kwa karibu mpango wa
Chelsea kutaka kusajili nyota wapya kikosi. Chelsea siku kadhaa nyuma
ilikataliwa kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira licha ya
kutoa ofa ya pound milioni 30.
January 21 stori kutoka express.co.uk
inaripoti kuwa klabu ya Chelsea ipo katika hatua za mwisho kukamilisha
mazungumzo ya kumsajili Alexandre Pato kutoka klabu ya Corinthians,
lakini kama itashindikana wataomba kumchukua kwa mkopo. Chelsea pia
inahusishwa kutaka kumsajili Carlos Bacca wa AC Milan na Saido Berahino
wa West Brom.
Stori za usajili za Chelsea hazijaishia
kwa upande wa kusajili pekee, bali wanatajwa kuwa na mpango wa kumuuza
Pedro Rodriguez mwishoni mwa msimu kurudi katika klabu yake ya zamani ya
FC Barcelona. Pedro ambaye amesajiliwa dakika za mwishoni za usajili wa
dirisha la majira ya joto.
No comments