Ziara ya pili Rais JPM kashtukiza tena, ya leo ni Hospitali ya Muhimbili Dar..
Headlines kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuanzia Ijumaa November 6 2015 siku ya kwanza ya Rais Dk. John Pombe Magufuli Ikulu, zilibebwa na stori ya ziara ya kwanza ya kushtukiza Wizara ya Fedha ambapo kuna baadhi ya watendaji alikuta hawapo Ofisini saa za kazi !!
Headlines nyingine inayoanza kukamata
nafasi kubwa mchana wa November 9 2015 kwa mara nyingine mitandaoni
inahusu ziara nyingine ya Rais JPM ambapo safari hii amekatisha
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo eneo la Upanga Dar es Salaam…
nako ameenda kimya kimya kwenye ziara ya kushtukiza vilevile.
#BREAKING: Rais JPM amefanya ziara nyingine ya kushtukiza Hospitali ya MUHIMBILI, atembelea wodini na kuongea na wagonjwa #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 9, 2015
Hiyo ndio Breaking News yenyewe na kilichonifikia kwa sasa, chochote kutoka hapo nitakusogezea anytime kuanzia sasahivi mtu wangu !!
No comments