Haya ni maneno ya Idris Sultan kuhusu ujio wa TV Show yake mpya BET…!
Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani… baada ya kuiwakilisha #255 vizuri kwenye shindano hilo kubwa la Africa, mafanikio mengi yamekuwa yakimfuata nyuma Idris Sultan!
Kama wewe ni miongoni wa watu wanaompenda na kumfuatilia Idris kwenye social networks basi hii good news ikufikie popote ulipo mtu wangu… Idris Sultan siku chache zilizopita alitudokeza kuhusu ujio wa TV Show yake mpya itakayo kuwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia channel ya BET pamoja na channel ya Vuzu za South Africa! Yote ikiwa ni sehemu ya kufanikisha ndoto zake za kwenda Hollywood, Marekani!
Staa huyo wa Tanzania ambae pia ni comedian mzuri sana alipata time ya kupiga stori na millardayo.com kuzungumzia nini kilimsukuma kuja na TV Show yake…
>>> “Kwanza
niliwekwa kwenye auditions ambazo nilitakiwa kufanya ili kuingia kwenye
Tv show ya ‘The Real Husbands of Hollywood’ show ambayo Kevin Hart
yupo, na auditions zangu zilitakiwa zifanyike tarehe 26th April… sasa
nikachelewa kuapply Visa ya kwenda USA kwasababu nilikuwa nafanya tours
nyingi ndani ya Africa bado kitu kilichopeleka auditions zangu kuwa
cancelled, na hapo ndipo niliposukunwa sasa kuanzisha reality show yangu
mwenyewe ili iwe rahisi kwa mimi kuonekana tena na kupata nafasi
nyingine ya kuingia Hollywood…” <<< Idris Sultan.
Sikuishia hapo, nikamuuliza Idris reality show yake itakuwa inahusu nini na kama show hio haitaathiri ndoto zake za kuwa Mchekeshaji mkubwa duniani…
>>> “Reality
show hainibadilishi mimi kama mimi kwasababu kwanza haina script, hiyo
show itakuwa inaonyesha sana sana what i do, kwa mfano sasa hivi mnaona
tu nafanya vitu tofauti lakini kupitia Reality Show yangu mtakuwa
mnaviona ninavyovitimiza, nimevifanyaje, nimepitia nini, na pia muda
gani niliwachekesha watu nusu kuzimia… vitu vyote hivi vitaonyeshwa, so
kwa ufupi itakuwa inaonesha maisha yangu halisi haswa upandae ambao
hamuuoni nyinyi kila siku… na haitanipotezea muda bali itakuwa
inaonyesha hustle yangu yote na vitu gani ambavyo navifanya mimi kama
mimi, na comedy itakuwemo humo humo haitaathiri chochote, comedy zangu
zote nitazifanyia humo humo!” <<< Idris Sultan.
Kama unakumbuka vizuri mtu wangu kuna kipindi Idris alianzisha kitu kinachoitwa ‘Hustle & Fame’ kwenye page yake ya Instagram, na inawezekana wengi wetu tumeona lakini hatujui ina maanisha nini… nikamuuliza Idris kama hili ndio jina la show yake mpya?, kwenye kupiga stori, staa huyo aliniambia haya…
Kwenye
show mpya ya Idris Sultan tegemea kukutana na hawa watu mtu wangu,
Samantha kutoka South Africa na Luis Munana kutoka Namibia wote kutoka
BBA 2014Sourc: Millard Ayo
No comments